Na Editha Edward, Michuzi TV, Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewasisitiza wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais ya jamhuri ya muungano wa Tanzania alioutoa hapo jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru kuwa wautumie Msamaha wa Rais kwa kutenda mema katika jamii wanazoenda kujumuika nazo kwani walipokuwa katika magereza hayo walijifunza mafunzo mbalimbali ikiwemo useremala ujenzi uashi kilimo poa walijifunza heshima na maadili hivyo ni vyema kuutumia vizuri Msamaha hyo
Mkuu wa gereza la uyui Omary Tensen amesema wafungwa hao Walionufaika kwa Msamaha wa Rais hapo jana kwa pamoja amewataka kuhakikisha hawarudi kufanya makosa hivyo wautumie fursa Hiyo kufanya kazi kwa bidii katika jamii zao ili kujikimu kiuchumi
Sonda Deus ambae ni miongoni mwa wanufaika wa Msamaha wa Rais amesema anamshukuru mhe, Rais Magufuli kwa kuwakumbuka walioko magerezani na anafurahi kuachiwa huru na kwenda kuungana na familia yake.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akizungumza leo na wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru. |
![]() |
Mkuu wa gereza la uyui Omary Tensen akizungumza na wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais |
![]() |
Baadhi ya wafungwa Walionufaika na Msamaha wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakiwa nje ya gereza tayari kwenda makwao |
![]() |
Gereza kuu la Uyui la Mkoani Tabora |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...