Wafungwa waliopatiwa Msamaha wa
Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania
wakiondoka katika gereza la Mbozi; Jumla ya waafungwa 96 Mkoani Songwe
wamepata msamaha wa Rais Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akiwa katika gereza la Mbozi ambapo wafungwa 96
Mkoani Songwe wamepatiwa Msamaha wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya
miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania

Wafungwa waliopatiwa Msamaha wa
Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania wakiwa
nje ya gereza la Mbozi kwa ajili ya kuondoka, Jumla ya wafungwa 96
Mkoani Songwe wamepata msamaha wa Rais Magufuli.
………………
Wafungwa 96
Mkoani Songwe wamekuwa miongoni mwa wafungwa Zaidi ya 5000 waliopatiwa
msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kufuatia maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika
yaliyofanyika jana jijini Mwanza.
Mapema leo Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefika katika gereza la
Mbozi ambapo wafungwa 45 wanapatiwa msamaha wa Rais huku wafungwa
wengine wakiwa katika Magereza ya Wilaya za Ileje na Songwe ambapo
amezungumza na wafungwa hao kabla hawapewa ruhusa ya kuondoka gerezani
hapo.
“Nimeingia
gerezani na kukuta wafungwa waliopata msamaha wa Rais Magufuli wakiwa na
furaha na wamempongeza sana Rais wetu, lakini pia wafungwa waliobaki
wamefurahia uamuzi wa Rais Magufuli wa kutoa msamaha kwani na wao wana
tumaini la kupatiwa msamaha siku za baadae.”, amesema Brig. Jen.
Mwangela.
Brig. Jen.
Mwangela ameongeza kuwa wafungwa waliobaki wamempa changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matatizo ya uhaba wa maji na
ucheleweshaji wa nakala za hukumu mambo ambayo ameahidi kuyashughulikia
haraka iwezekanavyo.
Kamishna Msaidizi
wa Magereza Laizack Mfaume Mwaseba amesema amekuwa akipokea malalamiko
ya ucheleweshaji wa nakala za hukumu kutoka kwa wafungwa na amekuwa
akiwasiliana na mahakimu ili waweze kuzitoa nakala hizo kwakuwa
ucheleweshaji huo unawanyima haki wafungwa ya kukata rufaa.
Ameongeza kuwa
pamoja na changamoto ya maji katika gereza hilo kuna changamaoto za
uhaba wa vitendea kazi na sare kwa wafungwa mambo ambayo tayari wamesha
yawasilisha kwa kamishana Mkuu wa Magereza kwa ajili ya utatuzi.
Mmoja wa wafungwa
wa gereza la Mbozi Victoria Adam amemshukuru Rais Magufuli kwa msamaha
alio mpatia na kumuombea kwa Mungu aendelee kumlinda huku akieleza kuwa
amejifunza mambo mengi alipokuwa gerezani na sasa anaenda kuwa raia
mwema.
Naye Fred Andrea
Daud ambaye amepata msamaha wa Rais Maguufuli amesema bahati aliyoipata
ya Msamaha ataitumia vizuri kwa kufanya kazi halali kwakuwa Vijana wengi
wamekuwa wakichagua kazi ambazo zinawaingiza katika matatizo
Ameongeza kuwa
magereza ni sehemu ya urekebishaji na yeye amerekebika hivyo anawashauri
vijana wote wafanye kazi halali ambazo hazitawaletea matataizo kwakuwa
kazi halali zipo nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...