Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WANANDOA
Kenneth na Mary Odipo waliofunga ndoa ya kifahari wiki moja iliyopita
huko Kisumu nchini Kenya wamejiua kwa kile kilichoelezwa ni mzigo wa
madeni uliokuwa ukiwaandama ukiwemo moja ya Benki DTB kutaka kuuza
nyumba ya wanandoa hao iliyopo Nyakenda Estate ili kufidia deni.
Mtandao
wa Kenya Today umeripoti kuwa wanandoa hao walijiua siku nne tuu mara
baada ya harusi yao na ni baada ya kugundua kuwa deni ambalo limetokana
na harusi limefikia shilingi ya Kenya 7.9 milioni ambayo ni sawa na dola
za kimarekani 78,000 na shilingi za kitanzania milioni 170.
Imeripotiwa kuwa kabla ya kutoa uhai wao waliacha ujumbe ulisomeka;
"Tumedharirika
na kuona aibu kuwa hatuwezi kuanza maisha yetu kwa furaha kwa kuwa
ninyi (watu) hamjatufurahisha kama tulivyotegemea" ulisomeka ujumbe huo.
Imeelezwa
kuwa wanandoa hao wametoa lawama kwa wageni waalikwa ambao walihudhuria
harusi hiyo na kula bila kuja na zawadi hali iliyopelekea kushindwa
kwenda kwenye fungate kama walivyopanga.
Imeelezwa
kuwa harusi hiyo ilifanyika katika hoteli ya nyota tano na kualikwa
watu wa hadhi ya juu waliotegemewa wangetoa zawadi za thamani na Fedha
nyingi.
Vilevile
imeelezwa kuwa kifo hicho ambacho kimegusa familia zote mbili, katika
siku ya harusi hiyo helikopta tatu zilikodiwa kubeba wanafamilia na
maharusi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...