Na, Editha Edward -Tabora.
Wakulima
wa zao la Tumbaku wilayani Kaliua Mkoani Tabora wametakiwa Kuanzisha
Mashamba ya Miti ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika vijiji vyao
Ametoa
Agizo hilo mkuu wa wilaya hiyo Abel Busalama wakati akizindua kampeni
ya upandaji Miti kwa Wakulima wa Tumbaku ndani ya wilaya hiyo
Amesema Miti ni muhimu kwa sababu inachochea uwepo wa mvua unasababisha udongo uwe na rutuba pamoja na kutunza uoto wa asili
Pia
amesisitiza ili kunusuru mazingira kutokana uharibifu mkubwa
unaochochewa na ukataji Miti kwa ajili ya shughuli za kilimo hivyo
Kila mkulima anatakiwa kupanda Miti katika mashamba yake
Busalama
pia ameagiza Wakulima wote wanaolima zao hilo kununua mashamba na
kupanda Miti ya kutosha ili kuhamasisha makampuni yanayonunua zao hilo
kuongeza idadi ya kilo watakazonunua
Aidha
amesema wataanzisha msako wa kukagua Kila shamba Kama Miti hiyo
itapandwa na endapo kwenye shamba atakapokutwa hajapanda Miti
atachukuliwa hatua ikiwemo kuzuiwa kupima hadi atakapopanda Miti
Katika
hatua nyingine ameipongeza kampuni inayonunua zao hilo la Tumbaku
wilayani humo ya Japan Tobacco International (JTI) kwa kusimamia
ipasavyo kampeni ya uanzishaji mashaba ya Miti kwa vyama vya Wakulima wa
Tumbaku katika wilaya hiyo
Kwa
upande wake Ofisa wa JTI Chrispin Mchafu amesema kampuni hiyo
imeanzisha kampeni ya upandaji Miti kwa vyama vyote vya Wakulima wa zao
hilo na kuongeza uzalishaji wa Tumbaku.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima.
Pichani ni baadhi ya wakulima wa Tumbaku wilayani Kaliua
Kila mmoja akiwa ameshikilia mche wa mti ili kwenda kupanda mashambani
mwao.
Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama akipanda mti katika moja ya shamba la mkulima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...