Na Editha Edward, Michuzi TV -Tabora
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewataka wananchi wa Mkoani Tabora kuhakikisha wanatoa pesa kwa ajili ya kuvuta Umeme wa REA kwa kila mwananchi ambaye hana Umeme nyumbani kwake na asiyefanya hivyo hatua kali zitachukiliwa
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara wilayani Kaliua mkoani humo ambapo amesema amesikitishwa na wananchi ambao nguzo za Umeme zimepita karibu na nyumba zao lakini wameshindwa kutoa pesa shilingi elfu ishirini na saba kwa ajili ya kuwekewa Umeme kwenye nyumba zao kwa kudai hali ngumu ya kiuchumi
"Umeme umeletwa kwa ajili yetu wananchi wa vijijini tutumie frusa hii ya Umeme kufungua viwanda vidogo vidogo kama mashine za kusaga na kukoboa itasaidia kuongeza kipato ch mtu na Taifa pia "Amesema Kalemani
Dkt. Kalemani amesema baada ya miezi sita atapita katika maeneo mbalimbali mkoani humo ili kukagua nyumba ambazo hazina Umeme kwa sababu Serikali imetumia gharama kubwa kufikisha nguzo vijijini na wananchi kushindwa kutumia frusa hiyo
"Tunakoelekea tutaanza kukamata watu ambao hawata vuta Umeme tunawatia kolokoloni wananchi vuteni Umeme bei ya umeme ni rahisi mno awamu hii ikipita Umeme kuufikisha nyumbani kwako itakua gharama "amesema Kalemani
Kwa upande wao wananchi Thomas Bukuge na Ngoko Mazwii wa wilayani humo wamesema wameyapokea maelekezo hayo ya Waziri na wamesema wameyapokea maelekezo hayo na wame ahidi watayatekeleza ka kuhakikisha wanavuta Umeme majumbani kwao
Hata hivyo Kalemani amewapongeza wakandalasi wanaosimamia mradi huo wa usambazaji wa Umeme kwa kufanya kuendana na wakati na kusambaza maeneo mengi pia amesisitiza ifikapo disemba 31 mwaka huu kila kijiji Niwe kimepata Umeme
Naye Meneja ambaye ni mkandalasi wa ujenzi Joseph Fumbuka amemuhakikishia Waziri kukamilisha kwa wakati usambazaji wa Umeme katika vijiji vilivyosalia kuhakikisha vinafikiwa na huduma hiyo
"Tutahakikisha tuna kamilisha kwa wakati kwani nguzo tumeshasambaza katika maeneo mengi kinachotukwamisha ni wananchi tunafikisha Huduma kwao lakini wanashindwa kulipia ili kufikishiwa Umeme majumbani kwao"Amesema Fumbuka.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa wilayani Kaliua Mkoani Tabora
![]() |
Wakandarasi wa Mradi Wa Umeme Wa REA wakimsikiliza Waziri Kalemani |
![]() |
Waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chemkeni. Picha na Editha Edward, Michuzi TV |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...