Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Mhe. Balozi Clavier kuwa, uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa ni wa muda mrefu ambapo hadi sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na taifa hilo.
Aidha, pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalijikita katika kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, kuongeza ushirikino wa maendeleo, kuimarisha uwekezaji, biashara pamoja na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akimfafanulia
jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na Mhe.
Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akimuelezea
jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na Mhe.
Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa Ufaransa nchini
Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo leo
katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsisitiza jambo Balozi wa Ufaransa
nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo
leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...