Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati akifungua kikao kazi cha maafisa hao cha siku mbili (tarehe 12-13, Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi akitoa maelezo mafupi kuhusu Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitambulisha washiriki wa Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho cha siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara cha siku mbili (tarehe 12-13,Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Michezo mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara cha siku mbili (tarehe 12-13 Desemba 2019) leo Jijini Dodoma. Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Michezo kwa Afya, Ajira na Maendeleo ya Viwanda”

(Picha na Shamimu Nyaki, WHUSM, Dodoma)

……………..

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Michezo kote nchini kulinda viwanja vya michezo na kutoa taarifa ya viwanja vya michezo vinavyobadilishwa matumizi hata kwa siri.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi cha Maafisa Michezo kinachofanyiki kwa siku mbili chenye lengo la kutathimini, kujadili na kuelekezana namna bora ya kuimarisha michezo na kutumia sekta hiyo kutangaza vivutio vya utalii nchini.

“Wapo baadhi ya Wakuu wa shule na walimu wanaozuia michezo shuleni na mnawajua, mnakaa kimya sasa wajibu wenu ni nini? Tambueni michezo sasa ni ajira ambayo ni mgodi na taifa lina vijana wengi simamieni vyema michezo,” Dkt. Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa kikao kazi hicho Dkt. Mwakyembe amekiagiza Chuo cha Michezo cha Malya kufanya utafiti wa kodi inayotokana na michezo mbalimbali inayofanyika nchini.

Naye Kaimu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo kukakikisha kikao kazi hicho kinakuwa endelevu na kufanyika kila mwaka. Aidha, aandae utaratibu wa kuwa na vikao hivyo kikanda vikiwa na lengo la kuwaandaa vijana waweze kushiriki michezo mbalimbali kitaifa na kimataifa.

“Kikao Kazi hiki kitatoa tathimini ya wapi tulipo, nini kifanyike pamoja na kutoa mwongozo wa kusimamia michezo mbalimbali na kutoa maelekezo kwa kuweka maazimio yatakayosaidia kupeleka michezo kuwanufaisha vijana maana michezo ni ajira,” alisema Dkt. Possi.

Aidha, Dkt. Possi aliwataka maafisa michezo hao kuzingatia mada ya uandishi wa maandiko ya udhamini katika michezo ambayo ni kichocheo cha kufanikisha michezo nchini kwani maandiko mradi hufanyika ni miongoni mwa kazi inayofanyika kila siku katika sekta ya michezo, hivyo ni vyema kuwa na ujuzi huo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo alitoa pongezi na shukrani kwa Makatibu Tawala Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kwa kuwawezesha maafisa michezo hao kushiriki kikao hicho kwa mikoa yote nchini imeshiriki. Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho Afisa Michezo kutoka Wilaya ya Mbarali Bw. Gerald Chiwaya aliishukuru wizara kwa kuandaa kikao hicho ambacho kimefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambacho kina washiriki 265 kutoka mikoa yote Tanzania Bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...