Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya
Dk Jamala Taibu kulia akibadilishana hati ya saini na Meneja wa Kanda
ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule kuhusu
mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na
Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya
Mnazi mmoja Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dk
Jamala Taibu kulia akitiliana saini na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam
Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine Haule mkataba wa makubaliano wa
Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla
iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Salome Mallamia akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad
Rashid Mohamed akitoa hotuba kuhusiana na umuhimu wa kupatiwa huduma ya
afya na Dawa wananchi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa
makubaliano wa Ununuzi wa Dawa baina ya Wizara ya Afya na Bohari kuu ya
Dawa MSD hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja
Zanzibar.
Wizara ya Afya
Zanzibar imetiliana saini hati ya makabdihiano ya ununuzi wa madawa kati
ya Bohari ya dawa Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuimarisha
huduma za afya nchini .
Utiaji saini huo
ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Jamala Talib
na Meneja wa Kanda ya Dare-es-Salaam Bohari kuu ya Dawa MSD Celestine
Haule ambao ulifanyika huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar .
Utiaji saini huo
ni wa muda wa miaka mitatu wenye lengo la kutoa huduma kwa kiwango
kinachohitajika katika kuboresha usafirishaji wa dawa na ununuzi kutoka
kiwandani.
Nae Waziri wa
Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa ni busara kutumia
huduma za ndani ya Tanzania kwa kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa
urahisi.
Aidha alisema
kuwa katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar ni
kuhakisha wananchi wanapatiwa huduma za matibabu bure na kuona
mashirikiano yanaimarika katika utoaji wa huduma.
Vilevile alisema
idadi imeongezeka ya wagonjwa kwa kuwepo ongezeko la wagonjwa ambao
wanahitaji huduma ya tiba na dawa hivyo Serikali imeongeza idadi ya
madaktari ili kuweza kutoa huduma.
Hata hivyo
alisema kuwa msimamo wa Serikali katika kuimarisha huduma zake imepanga
kununua dawa viwandani na sio kwa watu binafsi ili kuona dawa zinakuwa
na kiwango kinachohitajika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...