Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Mhasibu Mkuu fungu 50,Christopher Mkupama mshindi wa pili wa uandaaji Bora wa mahesabu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo.


Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imepata tuzo ya uandaaji bora wa mahesabu (Finacial statements) kwa mwaka 2018, kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu serikalini (IPSAS).

Tuzo hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wahasibu uliyofanyika Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo

Mkutano huo wa siku tatu uliowashirikisha wataalamu wa fani ya uhasibu zaidi ya 2,500 kutoka Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Halmashauri na Sekta Binafsi za hapa nchini pamoja na nchi za Kenya, Uganda,Burundi na Zambia, ulikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu kwa wataalmu hao kulingana na mabadiliko ya sekta hiyo yanayotokea ulimwenguni.

Aidha, Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwawezesha wataalam hao kuwa na lugha ya pamoja katika uaandaaji wa hesabu unaozingatia viwango vya kimataifa.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Fungu 50 Bw. Christopher Mkupama alisema Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imekuwa ikifanya vizuri katika uaandaji wa hesabu za mwaka kwa kipindi cha miaka minne mfufulizo na kupelekea kupatikana kwa tuzo hizo.

Alisema kuwa Tuzo hizo zimekuwa zikiiletea sifa Wizara ya Fedha na Mipango hasa Fungu 50 na kuchochea morali ya ufanyaji kazi kwa watumishi wa fani ya uhasibu.

‘’Nawashukuru sana viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na watumishi wa Kitengo cha uhasibu kwa kutufanya tuwe washindi wa pili kwa mara nyingine katika uaandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2018, tuzo hii ni shukrani kwa watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa mchango mkubwa wanaotoa kwa wahasibu katika uandaaji wa taarifa za hesabu za kila mwaka’’ alisema Bw.Mkupama.

Mkutano wa mwaka wa wahasibu ulianza tarehe 5 hadi 7 Disemba,2019 kwa kufunguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), Bw. Charles Kichere kwa niamba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpnago (Mb) na kufungwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...