Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack
Mbeteni (wapili kulia) akimkabidhi bango Mkurugenzi wa World Remit
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui kuashiria uzinduzi
wa huduma ya World Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa
kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine kushoto ni
Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera na Meneja Maendeleo
ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack
Mbeteni (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
huduma ya World Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea
pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine ni Mkurugenzi wa
World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui
na Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera.

Meneja Mkazi wa World Remit
Tanzania, Cynthia Ponera (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa huduma ya World Remit na Vodacom M-Pesa. Wengine
ni Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon
Kinyanjui, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na Meneja Maendeleo ya
Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.


Mkurugenzi wa World
Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya World
Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka
zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa M-Pesa,
Epimack Mbeteni na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.
**************************************
Desemba 17, 2019, Dar es salaam. Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na vinara wa kutoa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya mtandao WorldRemit , watawawezesha zaidi ya watumiaji wa M-Pesa Zaidi ya milioni 10 kupokea pesa moja kwa moja katika akaunti zao kutoka kwa marafiki na familia wanaosafiri na kufanya kazi nje ya nchi.
Huduma hiyo mpya inaongeza urahisi wa wapokeaji wa uhamishaji wa pesa mijini na vijijini kwani wanaweza kupokea pesa kutoka kwa jamaa na marafiki nje ya nchi moja kwa moja kwenye simu zao, bila kuhitaji kuwa na akaunti ya benki au kuunganishwa katika mtandao.
WorldRemit ni mojawapo ya vinara ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya uhamishaji pesa kupitia akaunti za simu ya mkononi, ambapo wameunganishwa na akaunti zaidi ya milioni 160 katika nchi 29. Mbali na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi, kampuni hiyo pia inatoa huduma za uhamishaji wa kibenki,huduma ya kuchukua pesa papo hapo na kuongeza muda wa maongezi nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd Epimack Mbeteni alisema, “Ushirikiano huu mpya na WorldRemit utatuwezesha kutambua malipo yanayofanyika kuja nchini Tanzania kila mwaka, utaongeza urahisi na uwezo kwa familia na marafiki nchini Tanzania kupokea pesa kupitia M-Pesa kutoka ulimwenguni kote na kufaidika na huduma za mawakala wetu zaidi ya 106,000 wa M-Pesa kote nchini, pamoja na mfumo wetu wa kibenki, unaowaunganisha na M-Pesa. Hii ni njia mojawapo ya kuboresha maisha ya wateja wetu “. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mwaka 2017 Wahamiaji wa kiafrika walituma dola bilioni 38 kurudi nyumbani ambapo mwaka huu inakadiriwa kufikia bilioni 39.6. Pesa inayotumwa kwa familia hutumika kuleta maendeleo na kufanya shughuli mbalimbali
za kiuchumi.
Malipo katika kiwango cha kidunia kwa Tanzania mara nyingi yanafanyika kupitia katika benki, ambapo bado kuna changamoto za gharama za kutuma, utaratibu wa utambulisho na muda unaotumika hadi kupata pesa.
“Ushirikiano huu utatoa suluhisho mbadala kwa kuwepo na wepesi na gharama nafuu katika kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa maana ya familia kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M–Pesa na wanaweza kuzitumia kwaajili ya kuleta maendeleo na katika shughuli nyingine za kiuchumi kama akiba na mikopo, huduma ya kutoa pesa zaidi,malipo ya kieletroniki na nyingine nyingi kutoka Vodacom,” aliongeza Epimack.
Kwa kutumia WorldRemit Watanzania wanaoishi katika nchi zaidi ya 50, ambazo ni pamoja na Amerika, Uingereza na Canada huokoa muda wao mwingi na pesa kwani hawahitaji kusafiri kwenda kwa wakala wa kuhamisha pesa na kulipa ada ya kutuma C2: VODACOM
GENERAL pesa nyumbani. Badala yake wanaweza kutuma pesa kwa njia ya mtandao wakati wowote kwa kutumia zana (app) au tovuti ya WorldRemit.
WorldRemit hailazimiki kulipa gharama zinazohusiana na mawakala wa maeneo katika nchi zinazohusika kutuma pesa, kampuni inapeleka akiba hizi moja kwa moja kwa wateja.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, gharama ya wastani ya kutuma £120 (~ $ 155) kutoka Uingereza kuja Tanzania ni karibu 9.5% Gharama ya WorldRemit kwa kiasi kama hicho inaanzia chini ya 2%. Kampuni hiyo pia kwa sasa imeondoa gharama katika miamala mitatu ya kwanza endapo watatumia namba ya utambulisho 3 FREE wanapofanya malipo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui alisema kwamba ushirikiano huu utapunguza ada za kutuma fedha, “uzinduzi huu utapunguza ada ambazo wateja wamekuwa wakilipa, hii ni kwa sababu kila kitu kinafanyika kidijitali,” aliongeza.
Meneja wa WorldRemit Tanzania, Cynthia Ponera, alisema, “Huduma yetu ya kuhamisha pesa kwa Tanzania inakua kwa zaidi ya asilimia 100, mwaka hadi mwaka, na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi ndiyo njia yetu kuu tunayoitumia kutuma pesa nchini.
Tunafurahi kushirikiana na Vodacom kupanua mtandao wetu zaidi na kuwaunganisha wateja zaidi ya milioni 12 wa M-Pesa kwenye huduma yetu ya kuhamisha pesa. Ushirikiano wetu utapunguza gharama ya kutuma pesa nchini na kuunga mkono mipango ya ujumuishaji wa kifedha kwa kuwapa fursa wapokeaji walioko vijijini katika kupata huduma hii rasmi ya uhamishaji pesa huko walipo”, alihitimisha bi. Ponera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...