Na Jumbe Ismailly IKUNGI
BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Mkoanai Singida limepitisha rasimu ya bajeti ya shilingi bilioni 36,853,533,471. 67 kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 zitakazotokana na makusanyo ya vyanzo vyake mbali mbali vya mapato ya ndani.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Ally Mwanga kwenye mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo uliokutana kujadili rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mwanga shilingi bilioni 1,976,820/= ni mapato ya ndani na kwamba kati ya fedha hizo shilingi 1,550,000/= zinatokana na mapato halisi na shilingi 426,000,000/= ni mapato zuiwa wakati ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na wadau mbali mbali ni shilingi 34,976,813,471.67.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa iwapo Halmashauri itakusanya mapato yake ya ndani vizuri kutakuwa na uwezekano wa kupanga shughuli za kukamilisha miradi mbali mbali ya maendeleo na ikichanganywa na fedha zinazotoka serikali kuu Halmashauri hiyo itakuwa na kiasi kikubwa cha fedha.
Mwenyekiti Mwanga hata hivyo alisisitiza kwamba katika bajeti ya fedha ya mwaka uliopita wa 2019/2020 Halmashauri ilipokea kiasi kikubwa cha fedha kwa miradi ya maji,lengo likiwa ni kumsaidia mwananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mwanga hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza madiwani wa kata kwenda kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kuu kwa kuangalia kiasi kilichopokelewa na kilichotumika kwa ajili ya kukamilisha vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari,vituo vya afya pamoja na zahanati ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Kuhusu watumishi wasiokaa kwenye vituo vya kazi,Mwenyekiti huyo aliwataka madiwani wajenge utamaduni wa kufanya ziara za kushitukiza ili waweze kuwabaini watendaji wanaokwepa kutioa huduma stahiki kwa waajiri wao badala ya kusubiri hadi mkuu wa takukuru aende kuwabaini watumishi wa aina hiyo .
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Haika Masawe licha ya kuwashukuru madiwani kwa kupitisha bajeti hiyo,lakini aliwataka pia wajumbe hao wa kikao kutambua kwamba kwa kiasi kikubwa uhai wa Halmashauri unategemea makusanyo ya mapato.
Aidha Masawe alisisitiza pia kuwa kutokana na kupitishwa kwa rasimu hiyo ya bajeti hivyo aliwahakikishia kwamba wataenda kuisimamia kwa vitendo bajeti hiyo na kuhakikisha kwamba fedha zitakazokusanywa zitakwenda kutoa huduma kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Edward Mpogolo aliwahakikishia madiwani hao kwamba serikali itaendelea kupeleka maendeleo kwa madiwani wote bila kujali itikadi za vyama vyao ambapo aliwaomba madiwani wote kutoa ushirikiano kwa wataalmu wanapokwenda kwenye maeneo yao.
Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Ikungi iliidhinishiwa na Bunge jumla ya shilingi 33,178,550,296.76 ambapo kati ya hizo shilingi 26,370,405,517.01 ni kwa ajili ya mishahara,shilingi 1,021,465,608/= kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 3,841,436,171.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hata hivyo hadi kufikia juni,30,mwaka jana Halmashauri hiyo ilikusanya shilingi 22,139,163,420.17 sawa na asilimia 64 ya bajeti yote wakati kwa makusanyo ya ndani Halmashauri hiyo ilikisia kukusanya shilingi 1,945,247,000/= na hadi kufikia juni,30,mwaka jana jumla ya shilingi 1,482,903,444.31 zilikusanywa sawa na asilimia 76 ya makusanyo yaliyokisiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Ally Mwanga akifunga mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...