Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, TG Matanga wa zimbabwe jijini Dar es Salaam.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Tanzania
inanufaika kiulinzi na usalama kutokana na kuwa mjumbe wa Shirikisho la
Wakuu wa Polisi wa nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

IGP Sirro ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, TG Matanga ambaye yupo nchini
kwa ziara maalum.

IGP Sirro amesema kuwa kutokana na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo,
Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia na kudhibiti makosa
yanayovuka mipaka yakiwemo makosa ya usafirishaji haramu wa
binadamu, wizi wa magari na dawa za kulevya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi Zimbabwe, Kamishna Jenerali TG Matanga, amesema yupo
nchini kwa ziara maalum ya kufanya tahmini ya utekelezaji wa maazimio ya
INTERPOL pamoja na maazimio ya SARPCCO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...