UBUNIFU uliotumika kutengeneza jukwaa kuu la Knowledge, Art na Networking (KAN) umekua kivutio kikubwa kwa wapenzi wa sanaa na burudani ya kupambwa na miamvuli ya rangi tofauti tofauti ikisindikizwa na michoro inayong’ara ikionesha watu wakicheza kwenye ukuta wa jukwaa.

Akizungumza kuhusu jukwaa hilo Mkurugenzi wa tamasha hilo Dave Ojay amesema kupamba jukwaa hilo na baadhi ya maeneo mengine kwa kutumia miamvuli kunaendana na kauli mbiu ya mwaka huu Maendeleo ni watu si vitu. Alisema, miamvuli imechukuliwa kama mfano wa mti unaoleta kivuli kwenye maisha ya watu.

Sanaa inayotumika kuchora maua yanayopambwa na rangi tofauti tofauti kwenye mwamvuli inawakilisha ‘art’ pamoja na vyuma vinavyofunguka na kufunga mwamvuli ukifunguka unawakilisha ‘network’ .

“Ubunifu wa kupamba kwa kutumia miamvuli inaendana na kauli mbiu ya tamasha ambapo sanaa ya kupata maua kwwenye miamvuli hiyo pamoja na vyuma vinavyoachana na kushikana wakati mwamvuli ukifungwa na kufunguliwa viinashiria nertworking,” alisema Ojay.

Kivuli cha miamvuli kinatasfiri maendeleo ya maisha ya mtu kama ilivyo kauli mbiu inayojadili mambo mbalimbali ya maendeleo yanahitaji pia kivuli ikiwa ni pamoja na malazi, makazi na chakula.

Msimu wa pili wa tamsha hili ulianza tarehe 22 na kufikia tamati jana ambapo wasanii wanne walihitimisha kufungwa kwa tamasha hilo.

Wasanii hao ni Fid Q, ktuoka Tanzania, Isabella Novella kutoka Mozambique, Victor Kunonga kutoka Zimbabwe, Bengatronics an Tear Drops kutoka Kenya.
 Msanii Saitoti Alakaila wa Warrios from The East akitumbuiza kwenye tamasha la KAN
 Msanii Lwanda Ataka wa Warriors from The East akitumbuiza wkati wa tamasha
 Msanii Sandra Nankoma kutoka Uganda akitumbuiza
 Msanii Amina kutoka Siti & The Band akitumbuiza kwenye jukwaa la KAN
Msanii Florence Shirima anayefanya spoken words kwenye jukwaa la KAN
Mpika kinanga wa Warriors from The East akiwa jukwaani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...