Wakati Suriya Tatakhun wa Thailand akitarajiwa kuwasili nchini Jumatano hii kuzichapa Salum Mtango kuwania ubingwa wa dunia wa UBO, mabondia 12 watazichapa kusindikiza pambano hilo.

Mtango na Tatakhun watazichapa Januari 31 kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga pambano la raundi 12 la uzani wa super feather.

Pambano hilo litatanguliwa na mengine sita ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia 12 wenye ushindani nchini.

Alen Kamote atazichapa na Haidar Mchanjo pambano la raundi sita la uzito wa kilogramu 61, Saidi Mundi atacheza na Hassan Mgaya pambano la uzani wa kilogramu 63.

Adam Yusufu atacheza na Bakari dunda, Mohamed Meme atazichapa na Saimon Zabron, Mchanja Yohana atacheza Sunday Kiwale na Idirisa Mannypaquiao atazichapa na Jey jey Ngotiko.

Promota wa pambano hilo, Ally Mwanzoa amesema maandalizi yamekamilika tayari kwa pambano hilo.

"Milango ya Mkwakwani itafunguliwa saa 6 Mchana kwa mashabiki kuanza kuingia, tunatarajia mapambano kuanza saa 10 jioni na lile la ubingwa kati ya Mtango na Mthailand litaanza saa 1 Usiku," alisema.

Alisema Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi akisindikizwa na mkuu wa mkoa wa Tanga.

"Mpinzani wa Mtango atawasili Dar es Salaam Januari 29 na moja kwa moja ataelekea Tanga na siku inayofuata atakutana uso kwa uso na Mtango katika zoezi la kupima uzito na afya," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...