Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Catherine Sungura akizungumza kuhusiana kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya  katika kuangalia mafanikio ya miaka mine ya Serikali ya awamu ya Tano walipofika katika  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali jijini Dar es Salaam.

 Mteknolojia mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali  Adam Mbugi  akionesha mashine za kisasa za upimaji wa sampuli mbalimbali ambazo serikali imewekeza katika mamlaka hiyo wakati timu ya waandishi wa habari na Timu ya maafisa wa habari walipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
 Mtaalam wa Teknolojia Daraja la Pili wa   Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali Leah Kalinga akichanganya sampuli wakati timu ya waandishi wa habari na Timu ya maafisa wa habari walipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko  akiwa katika picha ya  pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,jijini Dar es Salaam.
 
Na Chalila Kibuda,Michuzi Globu

MKEMIA mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema mamlaka ya maabara hiyo inampango wa kuanzisha mfumo wa kanzidata(Database) wa Taifa katika upimaji wa sampuli za vinasaba(DNA) utakaosaidia kurahisisha utambuzi wa miili iliyoharibika na watu wanaojihusisha uhalifu kwa kurahisisha uchunguzi na kutokutumia ndugu.

Katika kuanza mpango huo lakini pia serikali imewekeza mitambo na mashine mbalimbali katika kurahisisha utaoaji wa huduma ikilinganishwa na miaka ya nyuma pamoja na utanunuaji wa mifumo ya teknolojia ya habari katika ofisi hiyo.

Hata hivyo maabara ya mkemia Mkuu wa Serikali kwa Serikali ya awamu ya tano wameweza kuimarisha kanda tano katika utoaji huduma kwa wananchi pamoja na wadau.

Akizungumza na waandshi wa habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto katika kampeni ya Tumeboresha sekta ya afya kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano amesema Mfumo huo utatumiwa katika kurahisisha huduma za matibabu kwa kuangalia mfanano wa vinasaba na hiyo inatokana na serikali kuwekeza miundombinu katika maabara ya maabara ya mkemia Mkuu wa Seikali

Kanzi data hiyo itaangalia ulingano kwa ndugu wa karibu pia utatumika kwa watoto wa mtaani ambao wametelekezwa na wazazi wao.

“Tutumie kipindi cha miaka miwili kwamba hilo suala likamilike hilo linaenda hatua kwa hatua na inahitaji umakini mkubwa ambapo tuitashirikiana na taasisi zingine kama NIDA na RITA mfumo huo utasaidia utambuzi katika miili iliyoharibika lakini hii ni tofauti ukiwa na database badala ya kutafuta ndugu tunawapata kupitia mfumo huo pia itasaidia sana kwenye uhalifu mfano ubakaji ,mauaji ya kutumia silaha sasa tunapoanza kutumia mfumo wa database tutaweza kuwatambua.

Alisema faida nyingine ya mfumo huo pia utahusika katika suala zima la mirathi na uhalifu wa makosa ya jinai kama wizi,ubakaji,mauaji na majanga.

“Mfumo huo utaanza kwa watoto ambao wanazaliwa,katika mifumo ya matibabu na mahakamani.

Aidha amesema kuwa kwa kipindi cha miaka minne mapato ya mamlaka yameongezeka kutoka sh. bilion 9.342 mwaka 2015 na 2016 na kufikia bil 24.246 kwa mwaka 2018 hadi 2019. “Kwa uchunguzi wa kimaabara mafanikio yameonekana kwa asilimia 136.2 kutokana na usimamizi thabiti wa sheria zinazosimamiwa na mamlaka nyingine za serikali huku wakitoa ushirikianao katika majanga yanayoikumba Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...