Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela leo alhamisi tarehe 02 Januari 2020 ametembelea na kupata huduma kwa CRDB wakala aliyopo mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Akizungumza baada ya kupata huduma kwa Wakala ajulikanaye kwa jina la Gilbert George Gregory anayefanya biashara mjini humo, Bwana Nsekela aliwasihi wateja wa Benki ya CRDB kuwaamini na kuendelea kupata huduma kupitia mawakala wa Benki ya CRDB kwani ni sawa na kutembelea tawi lolote la benki ya CRDB; “Niendelee kuwasihi wateja wetu kuwaamini na kuwatumia mawakala wa benki ya CRDB kwani wanatoa huduma zote kama benki, pia wapo karibu zaidi na makazi na maeneo ya biashara ya wateja wetu, hivyo kuwapunguzia gharama za usafiri kufuata huduma au hata muda. Mwaka huu tumefanikiwa kuongeza idadi ya mawakala wetu kutoka elfu tano hadi elfu kumi na mbili ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinasogea karibu zaidi na wateja wetu” alisema Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akijaza fomu ya kutoa fedha alipotembelea kwa wakala wa Fahari Huduma, Gilbert George Gregory anayefanya biashara hiyo mjini Bukoba, leo Januari 2, 2020. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bukoba, Sydney Bakari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...