NA  YEREMIAS  NGERANGERA, NAMTUMBO

Njawala Ally (37) marehemu, mkazi  wa  kijiji cha Magazini  Wilayani  Namtumbo  mkoani Ruvuma  aliamua kujiua  kwa kunywa dawa  pamoja na pombe kali ili afe  baada ya kumkuta  mkewe  ndani ya nyumba  ya mpenzi wake  wakila chakula kilichoandaliwa  na mkeo.

Kwa  mujibu wa  shemeji ya marehemu  bwana  Daudi  Goliama alisema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na  homa  ya  kisukari kwa muda mrefu  akiwa anatumia dawa  pamoja na sindano ambapo  alizuiliwa kunywa pombe  wakati  akiwa anakunywa dawa hizo na madaktari  wa hospitali ya peramiho alikokuwa anatibiwa.

Aidha bwana  Goliama alidai mke wake  marehemu Mariamu Msola baada ya kuona hali ya mumewe alijishikiza kwa kijana  aitwaye  Beula Mohamedi na kumfanya mpenzi  wake huku  akijisahau kama anamume wa ndoa.

Tukio hilo lilitokea siku ya mwaka mpya  mchana  ambapo Mariamu alimwandalia mpenzi wake  chakula kizuri  wakati huo mumewe aliondoka  na kwenda  kwa majirani  kuzungumza .

Mumewe  akiwa na majirani  walimweleza  mwenzao  kuwa  mkeo ameelekea kwa mpenzi  wake  amebeba chakula  hali iliyomfanya marehemu kurudi nyumbani kuthibitisha kama yupo au hayupo na kwa kuwa marehemu Alisha kuwa na taarifa ya mahusiano yao ya kimapenzi alimwuliza mkeo  na alikataa kuwa hana  uhusiano naye .

Marehemu hakumkuta mkeo nyumbani  na kuamua kwenda nyumbani kwa mpenzi  wa mke wake huyo na kumkuta mkeo na mpenzi wake wakiwa ndani ya nyumba  ya mpenzi wake wakila chakula kilichoandaliwa na mkeo huyo  na ndipo alipomwuliza  mkeo kuwa ulikataa kuwa huna uhusiano  na huyo hapa umefika kufanya nini na kusononeka na kisha kurudi nyumbani kunywa dawa  pamoja na kunywa pombe kali ili afe.

 Baada ya kunywa dawa nyingi za homa za kisukari  pamoja na pombe kali alizidiwa huku akitamka bayana heri afe kuliko mambo anayofanyiwa na mkeo huyo na baada ya muda mfupi alifariki dunia.

Kaimu Afisa  mtendaji wa kata ya Magazini  bwana Ally Manoni alithibitisha kifo cha mtu huyo na kudai kuwa kifo hicho kimesababishwa na marehemu kunywa dawa nyingi za homa ya kisukari pamoja na pombe kali .

Marehemu  alizikwa  tarehe 2januari mwaka huu  katika makaburi  ya kijiji cha magazini ambapo  ameacha mke na watoto wawili mmoja wa kike darasa la pili na mmoja wa kiume anasoma chekechea shule ya Msingi magazini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...