Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Emma Lyimo (kulia)
akikabidhiana nyaraka na Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Luiz
Correia mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na mgodi huo kwa
ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa Sheria
za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi. Hafla hiyo
imefanyika leo Januari 13, 2020 katika Ofisi za Makamu wa Rais jijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka (kushoto) akikabidhiana nyaraka na Meneja
Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Luiz Correia baada ya utiaji saini wa
mkataba baina ya NEMC na mgodi huo kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo
ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya
Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake katika utekelezaji
wa shughuli za migodi.
Wajumbe kutoka Mgodi wa North Mara na Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakipitia nyaraka kabla ya kutiliana saini
kwa mkataba baina yao kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali
kuhusu uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za
migodi.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akisaini mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa
maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria
ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake katika
utekelezaji wa shughuli za migodi.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Mgodi wa North Mara, Bw. Tunzo Msuya akisaini mkataba wa baina yao kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu uzingatiaji wa Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake katika utekelezaji wa shughuli za migodi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...