Mwananchi Adrian Lucian Komba ameishukuru
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kumpatia matibabu baba yake Mzee
Lucian Anthony Komba na kupona kabisa.
Mzee Lucian Anthony Komba
alipokelewa MNH-Mloganzila tarehe 14 Januari, 2020 kutoka Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Morogoro baada ya kuanguka na kupata jeraha sehemu ya kichwa
lililopelekea hali yake kuwa mbaya.
Baada ya kupokelewa
hospitalini hapa alipatiwa matibabu na wataalam wa upasuaji wa mishipa ya fahamu
na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki tatu na kuruhusiwa kurudi nyumbani akiwa
amepona kabisa.
Akizungumza wakati wa
kushukuru Adrian Anthony Komba alisema baba yake amepona kabisa jambo ambalo
limewashangaza hata watu waliomuona baba yake wakati wa ugonjwa.
“Naishukuru Hospitali ya
Mloganzila na watoa huduma kwa matibabu haya kwa sababu nilimleta baba kwa
rufaa akiwa hajitambui leo namuona anaongea ni jambo la kufurahisha, hata watu
waliomfahamu wakati wa ugonjwa tuliporudi anaongea walimshangaa” amesema Komba.
Kwa upande wake Kaimu
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi amewashukuru
kwa kushukuru baada ya kupatiwa matibabu na kuwasihi wakawe mabalozi wazuri wa
hospitali kwani huduma bora zipo.
“Tunawashukuru kwa kurudi
kushukuru kwa huduma mliyopatiwa hospitalini hapa, nawasihi mkawe mabalozi
wazuri wa hospitali hii kwani huduma bora zipo” amesema Dkt. Magandi.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila,
Dkt. Julieth Magandi akizungumza na Mzee Lucian Komba (kushoto) pamoja na
mwanae Adrian Komba (kulia) waliofika hospitalini hapa kushukuru kwa matibabu
waliyopata.
Adrian Komba (kushoto) na
baba yake mzee Lucian Komba wakieleza jinsi walivyopatiwa matibabu hospitalini
hapo
Dkt. Magandi pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH-Mloganzila, Sr. Redemptha Matindi
wakipokea shukrani hizo.
Dkt. Magandi akiagana na Mzee Lucian Komba aliyepatiwa matibabu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kupona kabisa.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...