Mnamo
tarehe 02.01.2020 majira ya saa 16:05 jioni huko eneo la Meta-Igurusi
katika barabara kuu ya Mbeya/Njombe, Gari
lenye namba za usajili T. 956 DRT/T. 886
DRV aina ya Scania Tanker la Mafuta mali ya kampuni ya “world oil” lililokuwa limepakia mafuta aina ya Petroli kutokea Dar
es salaam kuelekea nchini Zambia likiendeshwa na dereva ISSA YUSUPH [35] mkazi wa Jijini Dar es Salaam lilipata hitilafu za
kiufundi siku ya tarehe 01/01/2020
majira ya saa 16:30 jioni na baadae liliungua
moto na kuteketea wakati wa harakati za kufaulisha mafuta kwenye gari hiyo kwenda
kwenye gari namba T 844 AWJ Trailer na
kusababisha majeraha kwa watu wawili.
Watu
waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya moto ni:-
1. JULIUS DAUDI
[30]
2. STANFORD MWAKYUSA
[45]
wote wakazi wa Igurusi Wilayani mbarali.
Aidha
katika ajali hiyo kulitokea uharibifu kwa gari namba SM 4633 aina ya Isuzu mali ya Jeshi la Zimamota na Uokoaji na gari
namba T 844 AWJ Trailer. Chanzo cha
ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya “water
pump”. Majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya igurusi kwa matibabu.
Imetolewa
na:
[ULRICH
O. MATEI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...