Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Nchini (TAEC )Nchini Profesa Lazaro Busagala
Dr. Remigius Kawala, Mtafiti na Mratibu wa Tafiti na Mafunzo wa Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini(TAEC)
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC
Mafunzo yakiendelea kama inavyoonekana katika picha katika Chuo Kikuu cha Sauti Kilichopo Jijini Mwanza
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sauti kilichopo Jijini Mwanza wakuwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na TAEC
Na.Vero Ignatus
Tume ya nguvu za Atomiki nchini imeendesha semina na kutoa Elimu juu ya matumizi ya Sayansi ya Teknolojia ya Nyuklia katika Maktaba ya chuo cha Mtakatifu Augustino (Sauti) Kampasi ya Malimbe
Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini Profesa Lazaro Busagala alisema jukumu la Tume hiyo ni Kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma, wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Prof.Busagala alisema Elimu hiyo ni muhimu katika sekta ya Afya Kilimo,mifugo,Viwanda,maji,ujenzi, pamoja na Kufanya utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbali mbali juu ya Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia
Awali Dr. Remigius Kawala, Mtafiti na Mratibu wa Tafiti na Mafunzo TAEC alisema mafunzo hayo yamejumuisha Wakufunzi,watafiti,wafanyakazi,wanafunzi ili kuwajengea uwezo juu ya udhibiti wa mionzi na uhamasishaji na uendelezaji wa matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia katika sekta mbalimbali .
Aidha mkutano huo ulilenga kuwaleta watafiti pamoja ili kubadilishana uzoefu kwenye nyanja ya Sayansi na Teknolojia sambamba na matumizi salama ya Teknilojia ya nyuklia mahaka pa kazi na jamii kwa ujumla.
Dkt.Kawala alisema kuwa Mafunzo hayo ni endelevu ambapo januari 28-2020 watakuwa Visiwani Zanzibar katika State University of Zanzibar (SUZA).
Amesema mafunzo hayo ni moja ya maandalizi ya mkutano wa maonyesho wa Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia unaotegemewa kufanyika tarehe 3-5 mwaka 2020 Jijini Arusha
Ifahamike kuwa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.7 yamwaka 2003 (The Atomic Energy Act. No.7 of 2003). Awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Taifa ya Mionzi (National Radiation Commission) iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.5 ya mwaka 1983 (The Protection from Radiation Act. No.5 of 1983)
Kulinga na na kifungu Na.6(1) cha Sheria ya Nguvu za Atomiki. Majukumu ya TUME ni Kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini,Kuhamasisha na kupanua matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...