Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba  akizungumza wakati wa kuzindua tuzo za Tehama na mawasiliano hapa nchini.
 Baadhi ya washiriki wakati wa uzinduzi wa tuzo za tehama na mawasiliano hapa nchini.
Katibu wa Umoja wa Wamiliki Blogs nchini, Krants Mwantepele akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tuzo za tehama na mawasiliano zitakazofanyika May 17, 2020 jijini Dar es Salaam.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mara ya kwanza imeandaa tuzo za kuwatambua watoa huduma za mawasiliano na Tehama hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema tuzo hizo zitakazofanyika Mei 17, mwaka huu huku ikisisitiza ni lazima kwa kila mwenye leseni kushiriki.

 Amesema kuwa  lengo la kuandaa tuzo hizo ni kuwatambua watoa huduma wao na kuchochea utoaji wa huduma bora za mawasiliano hapa nchini.

Amesema ni lazima kwa kila mtoaji huduma ambaye amepata leseni ya TCRA kushiriki katika tuzo hizo na kwamba kwa kutokufanya hivyo ni kukataa leseni hiyo.

"Utaratibu wa uandaaji wa tuzo hizi ulianza Julai mwaka jana lengo ni kila kada yenye leseni waweze kushiriki ili kujipima nafasi yao katika kutoa huduma," alisema Kilaba.

Pia amesema malengo mengine ya kuandaa tuzo hizo ni kuboresha utoaji wa huduma na kwamba wateja watapata fursa ya kupiga kura kwa mtoa huduma wake ili kuongeza alama katika mchakato huo.

Aidha  amesema Mei 17 ya kila mwaka ni Siku ya Mawasiliano na Habari duniani na kwamba wamekuwa wakiadhimisha kwa matukio mbalimbali hivyo, waliona umuhimu wa kuweka tuzo hizo ili kutambua michango ya watoa huduma wote Tanzania.

Hata hivyo amesema watoa huduma hizo wamechochea maendeleo ya sekta ya mawasiliano kwani matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) yanategemewa katika kukuza uchumi wa kati na wa viwanda.

"TCRA imetoa mwongozo unaotoa maelekezo na taarifa muhimu katika kushiriki kwenye tuzo hizo. Lazima mwenye leseni za TCRA kushiriki kwenye tuzo hizi ili mjipime na msipofanya hivyo, maana yake mnakataa leseni yetu," alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Tehama na Huduma TCRA, Connie Francis amesema tuzo hizo zinahusisha makundi 15 ambazo ni mtoaji huduma bora za simu wa mwaka, mtoaji huduma bora za mtandao, Televisheni bora ya Kitaifa ya mwaka, Televisheni bora ya Wilaya, redio bora ya kitaifa ya mwaka, redio ya Mkoa, Wilaya na ya Jamii, Televisheni Mtandaoni, Blogger na watoa huduma za usafirishaji mizigo na vifurushi.
Connie alisema wataanza kupokea maombi kwa njia ya mtandao za kushiriki kwenye tuzo hizo kuanzia leo hadi Machi 15, mwaka huu ambapo watazipitia na kuchagua maombi yaliyowasilishwa.

"Maombi haya yatumwe kwa http://ictawards.tcra.go.tz. baada ya kuyapitia maombi tutafungua dirisha la kupiga kura ambapo wateja wenu watapata nafasi ya kuwapigia kura kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili Mosi hadi 30, mwaka huu pamoja na kutuma ujumbe wa maandishi kwenda namba 15072," alisema Connie.

Nao watoa huduma kwa nyakati tofauti wamepongeza uandaaji wa tuzo hizo kwamba zitachochea ukuaji wa teknolojia nchini.
Umoja wa watoa huduma za simu ulisema maendeleo ya teknolojia yameongeza watu wanaotumia huduma za fedha kwa njia ya simu ambapo wamefikia milioni 20.

Katibu wa Umoja wa Wamiliki Blogs nchini, Krants Mwantepele amewataka kwenye blog kuhakikisha wanajidajili TCRA na kupata leseni ili kushiriki kwenye tuzo hizo kwani watapata fursa nyingi. Amesema elimu bado inahitajika kwa wamiliki wa mtandao hiyo kwani wengi hawajajisajili hivyo, kukiuka sheria zilizowekwa.

Tuzo hizo zinajumuisha makundi 15 ikiwemo mtoaji huduma bora za simu wa mwaka, mtoaji huduma bora za mtandao wa mwaka, Televisheni bora ya Kitaifa ya mwaka, Televisheni bora ya Wilaya, Televisheni Mtandaoni, Blogger na watoa huduma za usafirishaji mizigo na vifurushi kitaifa na Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...