MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), imefanya ziara ya kutembelea na ukaguzi wa viwanda 8 vya dawa za binadamu na mifugo vinavyoendelea kujengwa katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo aliambatana na wakaguzi wa viwanda kuangalia hatua zilizofikiwa katika ujenzi na kuendelea kutoa ushauri wa kitaalam ili kuwezesha viwanda hivyo kukidhi matakwa ya kisheria katika utengenezaji sahihi wa dawa (GMP).
Ziara hiyo ya siku tatu iliyoanza Januari 27-29 mwaka huu, ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano.
Viwanda vilivyotembelewa ni:-
Vista Pharmaceuticals Ltd na Kariuki Pharmaceuticals vilivyopo Zegereni, Kibaha, Hester Biosciences Africa Ltd na Biotec Pharmaceuticals vya mifugo vilivyopo Kibaha, Emedics Pharmaceuticals kilichopo Kerege Bagamoyo.
Pia Cure Pharmaceuticals Ltd kilichopo Kimbiji, Kigamboni, African Pharmaceuticals kilichopo Kisemvule Mkuranga na Alpha Pharmaceuticals Ltd kilichopo Mbangala Rangi tatu, Temeke.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (wa tatu kushoto) akipatiwa maelezo na watalaam wa ukaguzi wa viwanda katika moja ya kiwanda kinachojengwa.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja kwenye moja ya viwanda walivyotembelea katika ukaguzi.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...