Daktari wa watoto kutoka Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Amanda Anyoti akimwelezea balozi wa Israel
nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph
jinsi wanavyowahudumia watoto wenye matatizo ya moyo wakati balozi huyu
alipotembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za
matibabu ya moyo zinazotolewa.
Balozi wa Israel nchini mwenye
makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph akimjulia hali
mtoto Nembris Lubulo aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya
moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe.
Balozi Joseph alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma
mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Daktari bingwa wa usingizi na
wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge akimsomea balozi wa Israel
nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph
taarifa ya mtoto anayefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na
kuzibwa tundu la moyo wakati balozi huyo alipotembelea chumba cha
upasuaji. Mhe. Balozi Joseph alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya
kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa
Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded
Joseph alipotembelea taasisi hiyo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na: JKCI



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...