Na Nyamiti Kayora Dar es salaam
MKUFUNZI kutoka mtandao wa Jinsia na nishati endelevu Tanzania
(TANGSEN) Thabit Mikidadi, amesema moja ya sababu inayopelekea matatizo ya
ubakaji ni ukosefu wa nishati ya kupikia majumbani hususani vijijini.
Alisema
watu wa nishati wanaamini moja ya matatizo ya kijinsi, ikiwemo ubakaji yanaweza
kusababishwa na ukosefu wa nishati muhimu ikiwemo Kuni.
Thabiti
aliyaeleza hayo wakati akieleza kazi, majukumu na dhamira ya TANGSEN, kwa waandishi
wa habari wa za mazingira na nishati jadidifu nchini Tanzania, kuingiza masuala
ya jinsia katika sekta ya nishati, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salam.
Alisema
suala la nishati ni kitu muhimu katika sekta zote, hivyo waandishi wa habari
watakapoweza kuripoti vizuri habari za jinsia, katika nishati kunaweza kutokea
mabadiliko makubwa nchini.
“Sisi watu
wa nishati tunasema moja wapo ya matatizo ya kijinsia, kama ubakaji yanaweza
kusababishwa na ukosefu wa nishati, ni vizuri waandishi kutumia kalamu zenu
katika kuandika habari zenu”alisema.
Kwa upande
wake Caroline Gilbert kutoka mtandao wa Solar Sister Tanzania, alisema zaidi ya
wajasiriamali 4000 wamehamasiaka kufanya biashara za sola, ambapo kwa Afrika
watu Milioni 1.5 wanatumia nishari safi.
Alisema
asilimia 75%wananchi wa Afrika wanaoishi vijijini bado wanategemea mwanga wa
umeme wa sola, ambapo asilimia 26% ya wanawake wamejiingiza katika bishara za
ujasiriamali huku wakitegemewa nishati mbadala.
Alifahamisha
kuwa kumekuwa na vyanzo mbali mbali vya kupata mwangaza, vimekuwa ni hatari kwa
mazingira na afya ya watumiaji, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini wakati wa
ununuzi wa vitu hivyo.
Aidha Mkurugenzi
Mtendaji wa Nukta Africa Tanzania, Nuzulack Dausen, alisema mafunzo kwa waandishi wa habari yanalenga kujifunza mambo
mbali mbali ya msingi katika kuripoti habari za nishati Jadidifu.
Alisema
waandishi wameweza kujua mbinu mbali mbali za kisasa, katika kuripoti habari
kwa kutumia Takwimu, kutokana na mabadiliko ya dunia yalivyo hivi sasa.
“Ilikuwa ni
wiki ngumu ila wanahabari wataweza kuongeza kiwango cha uwandishi wao,
husuasani katika kuandika habari huku wakiingiza na takwimu ndani yake”alisema
Nuzulack.
Vilevile Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), John
Chikomo alisema mafunzo ya nishati jadidifu yamewashirikisha waandishi wa
habari 20 kutoka mikoa yote ikiwemo ni pamoja na visiwa vya Zanzibar, huku akiwataka kuhakikisha wanakuwa
waandishi bora katika masuala ya nishati nchini.
“Wataweza
kuripoti habari zinazohusu sekta ya nishati jadidifu kwa kina, pamoja na
kusaidia na kuhamasisha jamii jinsi ya kutumia nishati jadidifu kwa maendeleo
yao”alisema.
Hata
hivyo Makamu Mwenyekiti wa Tanzania
Renewable Association Prosper R. Magali, aliwataka waandishi wa habari kupaza
sauti zao ili kuwepo kwa sera na kanuni zinazohusiana na masuala ya nishati
jadidifu moja kwa moja.
Alisema ili
serikali kuweza kuwa na nishati mbadala ya kutosha nchini, lazima kuekeza fedha
za kutosha katika miradi hiyo ya nishati njini.
Kwa upande
wao waandishi wa habari wa masuala ya nishati jadidifu Tanzania, wamesema
mategemeo yao ni kuwa waandishi nguli nchini katika masuala ya nishati mbadala.
Waandishi wa habari za mazingira na nishati jadidifu wapo katika
mafunzo ya miezi sita yatakayowasaidia kujua na kufahamu vyema faida za nishati
hio na kutoa elimu kw aumma kupitia kalamu zao na ya yameandaliwa na Taasisi ya Nukta Afrika
Tanzania na Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa
kushirikina na HIVOS.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...