Na Zainab Nyamka, Globu ya Jami
KOCHA wa Yanga Luc Eymael ametoa mapumziko ya siku mbili kwa kikosi chake mara baada ya kumaliza kibarua cha Kombe la Shiriksho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) hapo jana.

Yanga wamechezea mchezo wao wa ASFC dhidi ya Tanzania Prisons  na kufanikiwa kuibuka na ushindi  wa goli 2-0 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Eymael amewapa mapumziko hayo ili kujiandaa na mchezo wa Mtibwa unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili.

Wachezaji hao watarejea tena mazoezini siku ya Jumatano ili kuanza kuwakabidili wakata miwa wa Morogoro Mtibwa  kwenye mchezo wa Ligi kuu VodacomTanzania.

Mchezo huo, utawakutanisha timu hizo mara ya pili ndani ya mwezi mmoja baada ya ule wa Mashindano ya Mapinduzi Yanga kuondolewa kwa hatua ya matuta kwenye mchezo wa nusu fainali.

Kocha Eymael ameweka wazi kuwa anahitaji kuona kila mchezaji anatimiza majukumu yake Uwanjani na kuhakikisha wanapata matokeo uwanjani.

Eymael huo ni mchezo wake wa tano toka kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo akicheza michezo mitatu ya Ligi akishinda mmoja na kupoteza miwili,  mchezo  mmoja wa Kombe la ASFC akifanikiwa kushinda na Jumapili hii  ataingia tena Kibaruani kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kuwa kwenye njia ya kuwania Ubingwa wa Ligi.

Yanga wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 28, Simba wakishika nafasi ya kwanza kwa alama 41, Azam alama 35 na Coastal Union ya tatu kwa alama 30.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...