Na Ripota Wetu, DODOMA

Wataalam wa kilimo cha umwagiliaji wameendelea na majadiliano Jijini Dodoma huku, wakibadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika Kilimo cha Umwagiliaji wakijikita zaidi katika shughuli za mradi huo,mafanikio na Changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo ambazo zinaweza kupelekea Mradi huo kuwa endelevu hata baada ya muda wake kufikia mwisho.

Wataalam hao walifanya mawasilisho ya Mpango kazi kupitilia utekelezaji wa mradi, kama vile kazi za upembuzi yakinifu katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo hufanyika kabla ya mradi kuanza na mradi kutekelezeka, jambo ambalo linapelekea ubora na uimara wa miundombinu ya umwagiliaji.

Sambamba na hilo, mawasilisho pia yalilenga katika majadiliano yaliyohusu tathmini na ufuatiliaji katika swala zima la matumizi na matunzo ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hasa katika eneo la matunzo ya miundmbinu hiyo.

Mradi huo ulianza kazi kwa awamu ya kwanza kutoka December 2010 mpaka June 2014, awamu ya pili kutoka August 2015 mpaka August 2019 na kuongezewa muda kuanzia September 2019 mpaka August 2020 ambapo mradi huo unaofadhiliwa na Shirika na Kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania utakwisha muda wake. 
 Washiriki katika mkutano wa wadau wa kubadilishana mawazo ya kitaalam kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima katika kilimo cha umwagiliaji,wakiwa katika makundi tofauti wakijadili kuhusu mafanikio, changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo na namna ambavyo mradi huo unaweza kutekelezwa na kuwa endelevu.
 Katika Picha Wataalam wakisikilza mawasililisho katika mkutano wa wadau wa kubadilishana mawazo ya kitaalam kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wataalam na wakulima katika kilimo cha umwagiliaji, unaendela Jijini Dodoma.
 Picha ikionesha wataalam washiriki katika mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa kujengea uwezo wakulima na wataalam katika masuala ya Kilimo cha Umwagiliaji wakijadili maswala ya utekelezaji wa mradi unaokaribia kuisha muda wake.
Bw.  Remigius Rushomesa, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani, kuhusu namna ambavyo mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika kilimo cha  umwagiliaji unavyoweza kuwa endeleevu hata baada ya kuisha muda wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...