Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kujadili hoja zenye maslahi mapana kwa taifa alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi  leo Jijini Dodoma.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akiwasihi wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) kuhahisha wanawasilisha hoja zitakazo saidia kuboresha sekta za wizara na utendaji  wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi  uliyofanyika leo jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa TUGHE  Tawi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Mfaume Said akiushukuru uongozi wa utawala wa wizara kwa kuboresha utendaji na kuwa karibu na wafanyakazi  pamoja na kusikiliza kero zao katika ufunguzi  wa baraza la wafanyakazi  uliyofanyika leo jijini Dodoma.
 Mtoa Mada kutoka TACAIDS  Dkt.George Matiko akitoa mada ya kuhusu  masuala ya Afya kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa kikao hicho cha baraza kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari,Utamduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeketi (wanne kulia)akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada yaufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika leo jijini Dodoma, watatu kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la wizara hiyo Bw.Mfaume Said.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiimba wimbo wa Solidarity wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza kilichofanyika leo jijini Dodoma,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo,Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Petro Lyatuu na Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Joyce Fisoo.

Na Anitha Jonas – WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa wizara hiyo kuwa wawazi katika mijadala ya mkutano huo  kwa mambo ambayo hayaendi  vizuri.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wenye lengo la kukumbushana, kuelimishana na kuweka mazingira bora ya utendaji kazi na kuweka umoja kati ya wafanyakazi  na viongozi wa menejimenti.

“Katika Baraza hili ningependa muwe wawazi katika mijadala ya mambo yote yanayokwamisha utendaji wa majukumu ya wizara lengo ni kuhakikisha mazingira ya utendaji yanaboreshwa na kazi zinafanyika kwa manufaa ya taifa kwa wizara hii inamambo mengi  yanagusa jamii moja kwa moja na hasa vijana tukiangalia sekta ya mfano Sanaa na Michezo,”alisema Dkt.Mwakyembe.

Naye  Kaimu  Katibu Mkuu  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi  aliwasitiza  wafanyakazi wa waadilifu, kuepuka ubadhirifu na kufuata kanuni na taratibu za utumishi  wa umma  kwa kufanya hayo itasaidia  kujenga mazingira yenye  manufaa kwa wananchi  na taifa kwa jumla.

“Mkutano wa baraza  ni muhimu kwani unawaleta wafanyakazi na menejimenti pamoja  hivyo basi kikao hichi kisitumimike  kutafuta umaarufu  badala yake utumike kujadili kwa kina  namna ya kuboresha  mazingira ya utendaji na mikakati ya itakayosaidia kuendeleza mbele sekta za wizara,’’alisema  Dkt.Possi.

Pamoja na hayo Dkt.Possi liwasisitiza wajumbe hao wa baraza kutoa hoja zenye tija na maslahi kwa wizara  huku akisema nimatarajio yake kuwa kikao hicho kitaibua fursa za namna ya kuboresha wizara na utendaji.
Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Tughe Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Mfaume Saidi aliushukuru uongozi wa wizara kwa kuboresha utendaji na kuimarisha kuimarisha ushirikiano kwa wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...