Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka wanafunzi ambao wamechaguliwa kidato cha kwanza katika shule maalum wakaendeleze vipaji vyao kwa kuweka jitihada katika masomo.
Amesema kuwa kuchaguliwa katika shule za vipaji hakuwafanyi washindwe kuongeza jitihada ili waweze kufika mbali zaidi.
Hayo ameyasema katika hafla yake maalum kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za vipaji maalum ndani ya Wilaya yake
"Msizembee mkajitahidi Kusoma ili mfikie malengo ,kwa ninyi watoto wakike msikubali mtu awakatishe masomo yenu lazima mfikie malengo yenu ya kufika mbali,"alisema Waryuba
Hata hivyo aliwapongeza wazazi na walimu kwa kushirikiana vizuri na kuwafikisha wanafunzi katika hatua ya kuigwa
"Katika hafla hii nimefarijika kuungana nanyi walimu,wazazi na wanafunzi ili kuwatia moyo watoto wetu ambao wamefanya vzr na kuwapa zawadi"alisema Waryuba
Katika halmashauri ya Tandahimba zaidi ya wanafunzi 30 wamechaguliwa kwenda shule za vipaji maalum.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akisistiza Jambo
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akimpongeza mmoja wa Wanafunzi ambao wamechaguliwa kidato Cha kwanza katika shule maalum wakaendeleze vipaji vyao kwa kuweka jitihada katika masomo.
Wageni waalikwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...