SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO  kupitia idara ya masoko imeanza zoezi la kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya na vijiji vya mkoa wa Tabora.
Lengo la utoaji huo wa elimu ni kuwaelimisha wananchi wanaopitiwa na mradi wa REA awamu ya tatu(REAIII) kufahamu taratibu za kuunganishiwa umeme pamoja kuchangamkia fursa za mradi kabla hazijaisha. Miongoni mwa wilaya ambazo tayari zimepitiwa na na sasa ziko kenye zoezi hilo la kupatiwa elimu ni wilaya ya Uyui, Sikonge, na baadae zitafuatiwa na wilaya ya Nzega na Igunga.
Wananchi hao pia walipatiwa elimu kuhusu kifaa cha UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao hususan zile zinye ukubwa wa wastani w avyumba viwili na sebule.
Wakizungumza wakati wa utoaji elimu kwenye vijiji vya Kagera, Ibiri, Msimba, Msuva, Mtakuja, Songambele na Kasandalala baadhi ya wananchi wamesifu jitihada za serikali za kuwaunganishia umeme kwa gharama ya shilling 27,000/= na tayari badhi yao wameshanufaika na mrafi huo wa umeme.
Afisa Uhusoiano na Huduma kwa wateja Tanesco mkoani Tabora  Bw. Lucas Swere akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya umeme wakati wa kampeni ya kuhamasisha wanavijiji kuunganisha umeme mkoani Tabora.
 Aafisa masoko kutoka TANESCO Neema Chalila Mbuja akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme na usalama wa umeme Kijiji cha Kagera na Songambele.
Aisa Masoko wa Tanesco, Bi. Neema Chalila Mbuja, (kushoto), akiungana na watoto wa kijiji cha Kagera na Songambele wakifurahia zawadi ya madaftari waliyopewa baada ya kujibu maswali yaliyoulizwa na wataalamu wa TANESCO baada ya kupatiwa elimu hiyo.


 Wanakijiji wakifuatilia kwa makini elimu iliyokuwa ikitoelwa kwao kuhusu masuala ya umeme.
Afisa masoko, Tanesco Bi. Jenifer Mgendi Maziku akitoa elimu ya namna ya kutumia kifaa kiitwacho UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...