Washindi wa shindano la ‘Scan, Lipa, Sepa” la Benki ya CRDB wakifurahia ushiriki wa taamsha la Sauti za Busara Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela akiwa na Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara Bwana Yusuf Mohamed na Mkuu Kitengo cha Kadi cha Benki hiyo Farid Seif katika Tamasha za Sauti za Busara Zanzibar. 
Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya CRDB Boma Rabala akiwa na washindi na wafanyakazi wa Benki hiyo katika banda maalum la kutolea huduma katika tamasha la Sauti za Busara.


Benki ya CRDB imeelezewa kuwa mdau muhimum katika kufanikisha tamasha kubwa la kila mwaka la kimataifa la Zanzibar lijulikanalo kwa jina la “Sauti za Busara”. Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo mjini Zanzibar juzi, Mkurugenzi wa Tamasha hilo Bwana Yusuph Mohamed alisema kuwa udhamini na uwepo wa Benki ya CRDB katika tamasha la mwaka huu umeleta hamasa kubwa katika kulitangaza zaidi tamasha hilo na pia kuhakikisha kuwa huduma za benki zinapatikana kwa wahudhuriaji wa tamasha hilo. 

“Tuna furaha kuwa Benki kubwa kama CRDB imejitiokeza na kuunga mkono tamasha hili ambalo linalenga kuibua vipaji, kutoa ajira na kuboresha utalii wa ndani. Kikubwa zaidi tunafurahushwa na kitendo cha Benki ya CRDB kuweka banda maalum la kutolea huduma za uwakala na ubadirishaji fedha za kigeni kwa washiriki wa tamasha hili” alisema Mohamed.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha biashara ya kadi cha Benki ya CRDB Bwana Farid Seif, alisema kuwa Benki ya hiyo iliamua kudhamini wa tamasha hilo ili kuunga mkono juhudi za kutangaza vivutio vya utalii nchini na kuibua vipaji vya sanaa ambavyo ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana.

Bwana Farid alisema pia ili kunogesha ushirki na ufahamu juu ya tamasha hilo, Benki ya CRDB Kupitia kampeni yetu ya malipo kwa kadi ijulikanayo kwa kama “Scan, Chanja, Lipa Sepa,’ imedhamini wateja wanne kushiriki tamasha hilo kwa kuwalipia gharama zote za usafiri na malazi kwa sika zote tatu za tamasha hilo. 

“Tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu kufanya manununzi na malipo kwa kutimia kadi zao katika mashine zetu za malipo yaani POS, zilizopokatika kila kona ya nchi ndani ya maduka, vituo vya mafuta, migahawa na sehemu mbalimbali za huduma na hivyo kuachana na utaratibu wa kutembea na pesa nyingi taslimu, ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wao” alisema Bwana Farid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...