



……………………………………………………
Akiwa katika
ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya Mwaka 2015 – 2020 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya ya
Micheweni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu
Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimetoa siku 30
kukamilishwa kwa mradi wa maji Wilaya Micheweni Pemba.
Hatua hiyo
imekuja baada ya Ndugu Polepole kufika katika eneo la Kilindini ambapo
kuna chanzo cha maji kinachopasa kupeleka maji kwa kilometa 4.6 hadi
eneo la Micheweni lakini mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na
kuelekeza kukamilika kwa haraka kwa mradi huo wa maji ili kurahisisha
huduma za kijamii na Kiuchumi katika Wilaya ya Micheweni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...