Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kipo tayari kushirikiana na chama chochote kwa kuzingatia maslahi ya mapana ya Tanzania nakuzingatia utaratibu unaokubalika kikatiba na kisheria katika mchakato wote wa kushiriki uchaguzi Mkuu wa 2020.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa maazimio hayo yamekuja baada ya kukuta kwa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha NCCR-Mageuzi yaliyofanyika Februari 19,2020.
Amesema kuwa katika kikao hicho cha halmashauri kuu ya taifa walikuwa na maadhimio mbalimbali ambayo ni katika kutekeleza malengo ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.
Katika madhumuni 18 ya chama cha NCCR-Mageuzi ni kutwaa hatamu za dola na kujenga jamii yenye demokrasia na maendeleo na ili kufikia lengo hilo ni kushiriki kusimamisha wagombea katika nafasi zitakazogombewa ambazo ni Udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo Mbatia amewaomba watanzania wote wenye nia njema ya maendeleo endelevu ya Tanzania kusikilizana, kushikamana na kushirikiana tukiwa watulivu na kuhakikisha nchi yetu iendelee kuwa na mfumo wa vyama vingi.
"NCCR-Mageuzi itaendelea kuelimisha na kuhamasisha watanzania umhimu wa katiba mpya yenye kukidhi mfumo wa vyama vingi vya siasa na kwa njia mbalimbali ikiwemo maridhiano ya kitaifa yenye misingi ya maelewano, maendeleo, umoja na amani katika makundi yote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Amesema Mbatia.
Wakati huohuo Mbatia amesema kuwa watatumia mfumo wao wa ndani ya chama katika kutimiza malengo kwa kutumia unyumbufu unaoendana na mabadiliko chanya ikiwemo kushawishi na kuhamasisha wananchi kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi ili kushiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...