NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO
AKIZUNGUMZA kwenye mkutanao wa uzinduzi wa zoezi la kulipakifuta jasho na machozi kwa wananchi wa kijiji cha Nambecha wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma katibu tawala bwana Aden Nchimbi aliwaagiza maafisa wanyamapori wilayani humo kufanya kazi walizosomea na sio vinginevyo.

Aden alisema serikali inatumia fedha nyingi kulipa kifuta jasho na machozi kwa wananchi walioathirika na wanyama waharibifu kila mwaka huku maafisa wanyamapori akiwaona wakiwa maofisini mwao na kazi kuwaachia askari wasaidizi wa vijiji (VGS) ambao nao wanadai kuzidiwa na makundi ya wanyama waharibifu.

“Tunashuhudia maafisa wanyampori wakiwa ofisini huku kero za wanyama waharibifu zikiongezeka ,naagiza maafisa wanyamapori kufanyakazi zao walizosomea badala ya kubaki ofisini na kazi zao kuwaachia askari wasaidizi wa vijiji” alisema katibu tawala huyo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nambecha bwana Selevesta Kadunda alimwambia katibu tawala huyo kuwa askari wasaidizi wa wanyamapori wa kijiji hicho hawawezi kukabiliana na makundi ya tembo yaliyopo katika kijiji hicho bila kupatiwa msaada wa askari wengine .

Afisa wanyamapori wa wilaya ya Namtumbo bwana Erenest Nombo alimhakikishia katibu tawala wa wilaya huyo kuwa wanaendelea kupambana na changamoto ya wanyamapori waharibifu katika vijiji vya wilaya hiyo licha ya uchache wa wataalamu wa wanyamapori

Bwana Nombo aliwasisitizia wananchi kuendelea kutumia mbinu za kuwafukuza wanyama zilizofundishwa ikiwemo ya kilimo cha ufuta, pilipili na matumizi ya oili chafu badala ya kuacha na kuwategemea askari pekee ambao ni wachache.

Nia njema ya Serikali ya awamu ya Tano ya kupambana na majangili na kulinda wanyamapori hali hiyo imesababisha ongezeko la wanyamapori ambao kwa sasa wanahatarisha maisha ya wananchi na mali zao

Zoezi la kulipa kifutajasho na machozi kwa wananchi wa wilaya ya Namtumbo kwa mwaka 2018 serikali ilitumia kiasi cha shilingi 22,175,000 na kuwalipa wananchi 123 katika vijiji 7 vya wilaya hiyo na mwaka 2019 wananchi 350 walilipwa kifuta jasho na machozi ambapo serikali ilitumia kiasi cha shilingi 48,045,000 katika vijiji 15 vya wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...