Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Ndg. Julius Mtatiro, amevitaka vyama vya ushirika na vyama vya akiba na mikopo kuzingatia taratibu na sheria katika utendaji kazi wao na kuacha kufanya kazi kwa kwa mazoea.

Ndugu Mtatiro ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku ya tatu ya vyama vya ushirika na vyama vya akiba na mikopo yaliyoandaliwa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Shirika la Ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (Tawi la Ruvuma) na Maafisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru.

DC Mtatiro ameonya michezo michafu na vitendo visivyokubalika na kuwataka wana ushirika wote kuwa na msimamo wa kujali wakulima na ukuaji wa ushirika na vyama vya ushirika.

Mtatiro amewakumbusha  viongozi wa Ushirika kuwa serikali ya wilaya iko macho na itahakikisha wale waote wanaojaribu kuyumbisha ushirika katika chaguzi zinazoenda kuanza hivi karibuni wanachukuliwa hatua bila kuonewa haya.

Mtatiro amewataka viongozi wa ushirika kuuchukulia kama sekta muhimu mno na yenye tija akitolea mfano kuwa wilaya ya Tunduru kwenye msimu ulipita 2018/19 wakulima  ameweza kupata jumla ya shilingi bilioni 61kwenye korosho na msimu wa 2019/20 wakulima wamepata shilimgi bilioni 67 huku wakitarajia kupata shilingi bilioni 5 katika ufuta baadaye mwaka huu.

Mtatiro amesisitiza fedha zote hizo zinapita katika vyama vya ushirika na vyama vya msingi na amewataka wadau wa vyama hivyo kuhakikisha wanawachagua viongozi wenye uwezo wa kulinda na kutetea maslahi na fedha za wakulima.

Ni kutoka hapa ukumbi wa Cluster Tunduru, Alhamisi 20 Februari 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...