Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),
akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Balozi Ali Davutaglu
wakati mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la
Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati walipomtembelea
na kufanya nae mazungumzo leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
Salaam

Balozi wa Italia nchini Mhe.
Balozi Roberto Mengoni akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),
wakati mabalozi hao walipomtembelea Naibu Waziri na kufanya nae
mazungumzo

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),
akiwaeleza jambo mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus
(UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati
walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),
akiwa ktk picha ya pamoja na mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting
for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa
…………………………………………………
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),
amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano (5) hapa nchini
wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya
Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa.
Dkt. Ndumbaro amekutana na
mabalozi hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
ambapo ujumbe huo umewahusisha, Balozi wa Italia nchini Mhe. Balozi
Roberto Mengoni, Balozi wa Hispania nchini Mhe. Balozi Fransisca Pedros,
Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnel, Balozi wa Uturuki nchini
Mhe. Balozi Ali Davutaglu, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini
Mhe. Tae-ick Cho.
Pamoja na mambo mengine,
majadiliano hayo yalijikita kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
ulinzi na usalama wa Umoja wa Mataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...