Waziri wa maendeleo na biashara ya nje wa Finland Bw. Ville Skinnari na ujumbe wake alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Wizarani hapo, Jijini Dodoma leo tarehe 24/02/2020 
………………………… 

Waziri wa Maendeleo na Biashara ya kimataifa wa Finland Bw. Ville Skinnari amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Mendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu kuhusu maendeleo na usawa wa jinsia hapa nchini.
Akizungumzia masuala ya Jinsia, Katibu Mkuu Jingu amesema Serikali imechukua hatua madhubiti kuboresha usawa wa kijinsia na haki ya mtoto wa kike. 

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewekeza katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na masuala ya uongozi. Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkakati kukabiliana na mimba katika umri mdogo na kupinga mila zilizopitwa na wakati ikiwemo ukeketaji. 

Aidha, ameongeza kuwa sera ya Taifa ni kushirikisha wananchi katika jitihada za kukabiliana na vikwazo vilivyopo. Dkt. Jingu amesema Serikali katika ngazi mbalimbali za uongozi imeunda kamati maalum za kulinda na kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa. 

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo na Biashara ya Kimataifa kutoka Finland Bw. Ville Skinnari amesema nchi yake inaunga mkono juhudi za Tanzania kupambana na changamoto zilizopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...