*Uchunguzi huo ni mara sita ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,Arusha
KUFUATIA hatua ya serikali kupiga marufuku kemikali zisizofaa pamoja na usimamizi thabiti wa kupambana na dawa za kulevya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kaskazini (GCLA) imesema kumekuwa na ongezeko la uchunguzi wa sampuli kutoka sampuli 512 kwa mwaka 2016,2017 kufikia sampuli 3,232 kwa mwaka 2019,2020.
Hayo aliyasema Meneja wa GCLA kanda ya Kaskazini Christopher Anyango wakati akiongea na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wanaoendelea na kampeni inayoangazia mafanikio katika sekta ya Afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano inayojulikana kama Tumeboresha sekta ya Afya.
Anyango alisema ongezeko la upimaji wa sampuli kumechangiwa na uimarishwaji wa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali.
Amesema kwa mwaka 2016,2017 viwanda vilivyosajiliwa kushugulika na kemikali ni 100 lakini sasa 2019,2020 wamesajili viwanda 250.
Aidha katika kipindi cha Rais Dkt.John Pombe Magufuli wamesajili viwanda 150.
Katika utoaji wa vibali vya kutumia kemikali Anyango amesema GCLA kwa mwaka 2016,2017 wametoa vibali 2,000 na kwa mwaka 2019,2020 walitoa vibali 2,172.
"Kwa mwaka 2016,2017 uthibiti wa kemikali kwa upande wa mipakani haukuwa wa kiwango kikubwa kwasababu tulikuwa na mtumishi mmoja pekee aliyekuwa katika mpaka wa Namanga ,uingizwaji wa kemikali ulivyoongezeka,serikali ilitutengea bajeti iliyotuwezesha kuajiri watumishi,ambao wapo katika mipaka mikubwa mitano ya kanda ya kaskazini"alisema.
Amesema kuajiriwa kwa watumishi hao,kumewasaidia kwani GCLA imekuwa ikipata taarifa nyingi zaidi tofauti na miaka ya nyuma, ambapo walikuwa wakiwatumia maofisa afya kuwapatia taarifa zinazohusu kemikali katika mipaka.
Akizungumzia maboresho ya GCLA alisema wameboresha mfumo wa utoaji wa vibali kwa njia ya mtandao jambo linalorahisha utoaji wa vibali pamoja na ukaguzi.
"Hakuna watu wanaokuja ofisini kwetu kuomba vibali bali wanaingia kwenye mtandao na kuomba vibali,ndani ya muda mfupi tunaangalia ombi lake na kupata majibu kwa muda mchache"alisema.
"Pia tuna mpango wa kuanza kupima sampuli zote zinafikishwa hapa kwa wingi "alisema.
Kwa upande Mtaalamu wa Maabara Saile Maregesi alisema maabara ya GCLA kanda ya kaskazini imekuwa msaada mkubwa katika kusaidia upimaji wa sampuli za seli kwa watu waliofanyiwa ukatili wa kijinsia kama ubakaji.
Mteknolojia wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Kanda ya Kaskazini Saile kurata akionesha kuhusiana na Uchunguzi wa Maabara wa sampuli mbalimbali katika maabara ya Kanda ya Kaskazini.
Jengo la Zamani la mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA Kanda ya Kaskazini.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Christopher Anyango akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto walipofika katika Ofisi ya Kanda hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya Tano.
Uwekezaji wa Serikali ka mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika Kanda ya Kaskazini






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...