Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Dkt. Anna Mghwira akisikiliza maelezo toka kwa Mrakibu msaidizi wa
Uhamiaji, Sale Sule alipotembelea banda la Uhamiaji katika maonesho ya
wiki ya sharia yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mahakama
katika manispaa ya Moshi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Dkt. Anna Mghwira akipata maelezo ya Pasipoti mpya za Kielektroniki
toka kwa Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule wakati alipotembelea
banda la uhamiaji kwenye ufunguzi wa wiki ya sharia mkoani Kilimanjaro.
Mrakibu wa Uhamiaji Grace Malagila
akishiriki kikamilifu mazoezi ya viungo ya pamoja yaliyoongozwa na Mhe.
Dkt Anna Mghwira (hayupo pichani) kabla ya ufunguzi rasmi wa wiki ya
sharia. Wadau mbalimbali walishiriki katika mazoezi hayo, vikiwemo
vyomba vya ulinzi na usalama.
Mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji
Dorothy Ngai akifafanunua jambo kwa moja ya wadau waliotembelea banda la
Uhamiaji katika maonesho ya wiki ya sharia. Pembeni ni Koplo Vedastus
Ng’aire.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji
Octavia Makwawa akifafanunua jambo kwa moja ya wadau waliotembelea banda
la Uhamiaji katika maonesho ya wiki ya sharia. Pembeni ni Konstebo
Innocent Mshana.
Wadau mbalimbali wakishiriki
matembezi maaulu yaliyoandaliwa na Idara ya Mahakama katika ufunguzi wa
maadhimisho ya waiki ya sharia Mkoani Kilimanjaro. Idara ya Uhamiaji kwa
Kushirikiana na Chuo cha Uhamiaji – TRITA, walishiriki kikamilifu
katika matembezi hayo.
……………………………………………………
KAULIMBIU:
“uwekezaji na biashara jukumu la mahakamana wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji”
Na Afisa Uhusiano & Itifaki- TRITA
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.
Dkt. Anna Mghwira ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wote bila kujali
uwezo wa kipato kwa wanaokuja kupata huduma za kimahakama katika ofisi
husika. Mhe. Mghwira amesema hayo jana tarehe 31 Januari 2020 wakati wa
ufunguzi rasmi wa wiki ya Sheria Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, katika maadhimisho hayo
yaliyotanguliwa kwa maandamano yaliyoshirikisha taasisi mbalimbali
vikiwemo vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Idara ya Uhamiaji
yalipambwa kwa matukio mbali mbali kama vile mozoezi ya pamoja,
matembezi ya umbali wa kilometa tatu pamoja na ufunguzi rasmi wa mabanda
ya maenesho.
Mhe. Mkuu wa Mkoa alipata nafasi
ya kutembelea banda la Uhamiaji, ambapo alipewa elimu kuhusiana na
utolewaji wa pasipoti mpya za kielektoniki na mikakati mbalimbali
aliyowekwa na Idara ya Uhamiaji katika kupambana na wimbi la wahamiaji
haramu.
Mhe. Mghwira alifurahishwa na
maelezo yaliyotolewa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule ambaye
sharia, kanuni na miongozo huku akisisitiza udhibiti wa mipaka na
wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia kwa wingi pia ni Mwanasheria
wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro.
Kabla ya kumaliza ziara yake
katika banda ya Uhamiaji, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna
Mghwira aliitaka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro kufanya kazi kwa
kuzingatia kupitia njia za panya hapa nchini wakitokea nchi jirani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...