RAIS wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu Jijini Dar es Salaam hali iliyofanya madhari ya Ikulu kupendeza na kuvutia.
Wanyama waliopo katika bustani hizo ni pamoja na Pundamilia, Pofu, Swala, Digidigi, Tausi, Mbuni, Tumbili, Kanga, Batamaji na wengine.
Awali wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa wakati wa Uongozi wa Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na baadaye walitoweka hadi mwaka 2017 walipoanza kurejeshwa na Mhe. Rais Magufuli.
Katika maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam hivi sasa kuna ongezeko kubwa la ndege aina ya Tausi ambao wanaonekana kulipamba Jiji la Dar es Salaam. Picha na Ikulu.
Wanyama wakijivinjari Ikulu.
Wanyama wakijivinjari Ikulu.
Mbuni
Pundamilia.
Tausi.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...