WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, ameipongeza Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kwa kuandaa Tamasha la Mama Lishe ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa mama lishe katika kuleta maendeleo.
Jafo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa halmashiri zote nchini ambao wataoshindwa kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanawake, walemavu na vijana watachukuliwa hatua ikiwemo ya kutumbuliwa.
Jafo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa halmashiri zote nchini ambao wataoshindwa kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanawake, walemavu na vijana watachukuliwa hatua ikiwemo ya kutumbuliwa.
Akizungumza kuhusu tamasha hilo la Mama Lishe, mbele viongozi na wananchi wa Wilaya ya Kisarawe, Jafo amesema ni ubunifu unaostahili kupongezwa kwa kuwa pqmoja na mambo mengine unahamasisha ujasiriamali, lishe bora na kupata mtandao wa wadau kufanya nao biashara.
"Niwapongeze sana wilaya ya Kisarawe mkiongozwa na Mkuu wa Wilaya yenu, jambo hili ambalo mmelifanya ni la kwanza kufanyika nchini na linastahili kuigwa na wilaya nyingine.Mmeonesha kwa vitendo katika jitihada za kutambua makundi mbalimbali yakiwemo ya wanawake ambao wanajihusisha na mama lishe,"amesema Jafo.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuhusu asilimia 10 ambayo inatakiwa kutolewa na halmashauri kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu kwa Wilaya ya Kisarawe wanajitahidi sana huku akisisitiza kuhusu tamasha hilo ni vema likawa linafanyika kila mwaka."Wilaya ya Kisarawe hadi sasa imetoa mikopo kwa makundi hayo yenye thamani ya sh. milioni 542.480 katika kipindi cha kuanzia oktoba 2015 hadi januari 2020".
Hivyo ametumia nafasi hiyo kutoa maagizo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kwa ajili ya makundi maalumu ambayo yanapaswa kupewa fedha hizo kama maagizo ya Serikali yanavyoelekeza.
"Nawaambia wakurugenzi ambao hadi Juni 30, mwaka huu watakuwa hawajatoa mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu kutokana asilimia 10 ya mapato ya ndani nitaandika barua yenye mapendekezo kwenda Rais ili wachukuliwe hatua.
"Ikitokea wametumbuliwa wasimtafute mchawi kwani watakuwa wamesababisha wenyewe kwa kushindwa kutoa mikopo hiyo ambayo ni jambo la lazima," amesema.Kwa mujibu wa Jafo katika suala la asilimia 10 ya mikopo kusaidia makundi hayo Serikali haifanyi utani kuhusu kuwawezesha wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ameeleza jitihaa ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo ya wananchi huku akisisitiza katika wilaya hiyo kuna mambo mengi makubwa ya maendeleo yamefanyika.
Wakati huo huo amesema kuwa hadi sasa Sh.milioni 542.480 zimetolewa kuanzia Oktoba 2015 hadi Januari mwaka huu ambapo vikundi vya wanawake vilikopeshwa sh.279.686 sawa na asilimia 51.5 vijana sh. Milioni 251.294 sawa na asilimia 46.3, walemavu sh. Milioni 11.5 sawa na asilimia 2.5.
Katika hatua nyingine Jokate amesisitiza magari yote ya abiria kutoka vijijini ndani ya wilaya hiyo kumalizia safari zao katika kituo kipya cha mabasi kilichopo Kisarawe mjini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Mussa Gama amewataka wajasiriamali hasa mamalishe kujitokeza kuomba mikopo inayotolewa na halmashauri na taasisi zingine ili kujiimarisha zaidi.
Wakati huo baadhi ya mama lishe akiwemo Sikuzani Masudi kutoka Kijiji cha Msanga, amesema fursa iliyotolewa na wilaya hiyo ina nia njema na anaamini itasaidia kuwakomboa wajasiriamali walioko vijijini.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zainab Vullu (wa kwanza kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgallu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Joketi Mwegelo wakiwasalimia baadhi ya mama lishe wa wilaya hiyo wakati wa tamasha la Mama Lishe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akizungumza wakati wa Tamasha la Mama Lishe ambalo limeandaliwa na Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ikiwa ni mkakati wa kutambua na kuthamini mchango wa Mama Lishe katika maendeleo ya wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza kuhusu maendeleo ambayo yamepatikana kwenye Wilaya hiyo pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zimepatiwa ufumbuzi wake wakati wa Tamasha la Mama Lishe lililofanyika wilayani humo
Naibu Waziri wa Nishati(katikati) Subira Mgallu akizungumza mbele ya Mama Lishe wa Wilaya ya Kisarawe mkoani wakati wa tamasha hilo ambalo lilishindanisha mama lishe kupika vyakula na mshidni wa kwanza hadi wa tatu walipatiwa zawadi mbalimbali zilizoandaliwa na Wilaya ya Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumzia Tamasha la Mama Lishe wilayani humo ambapo pamoja na mambo mengine amesema tamasha la aina hiyo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo na lengo ni kuwatambua na kuwathamini mama lishe wote ikiwa sehemu ya jitihada za Serikali katika kuhamasisha lishe bora kwa wananchi.
Baadhi ya Mama Lishe katika Wilaya ya Kisarawe wakiendelea na mapishi wakati wa Tamasha la Mama Lishe lililofanyika wilayani humo ambapo waliopika vizuri walipatiwa zawadi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu (katikati) akizugumza wakati wa tamasha la Mama Lishe ambalo limefanyika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(aliyevaa kofia) akisalimiana na majaji ambao wamepewa jukumu la kutafuta washindi wakati wa Tamasha la Mama Lishe ambapo waliopika vizuri kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na majaji waliibuka washindi.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria Tamasha la Mama Lishe wakifuatilia kwa karibu tamasha hilo wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa tamasha hilo.
Naibu Waziri wa Nishati (mwenye kilemba cheusi) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo wakati akielezea zawadi mbalimbali yakiwemo beseni, vikombe, vijiko na sahani ambazo zimetolewa kwa kwa washindi wa Tamasha la Mama Lishe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...