Viongozi wa SACCOS Kanda ya Kati wakishiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.


Na Ismail Luhamba, Singida


ZAIDI ya SACCOS 90 za Mikoa ya Kanda ya Kati zimepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa viongozi wa SACCOS yatakayosaidia kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa leseni za vyama vyao.

Mafunzo hayo yanayofanyika nchi nzima yametolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini yatawezesha viongozi wa SACCOS hizo kutambua na kutumia mifumo ya kifedha katika SACCOS zao.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika hapa nchini JOSEPHAT KISMALALA amesema licha y mafunzo hayo kuwajengea uwezo lakini pia yatapunguza wakopeshaji haramu kwenye SACCOS.

‘’Nasisitiza SACCOS nchini kuhakikisha wanakata leseni kabla ya hatua kali za kisheria kuchuliwa kwani hii ni sheria ya benki kuu ya Tanzani kila SACCOS kuwa na leseni, na sisi kama serikali hatupendi tufike huko matumini yangu kila SACCOS zitakata leseni kwa wakati ili kila mtu awe ametimiza wajibu wake.

Kwa upande wa Mrajis Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Singida Bw. Thomas Nyamba alisema anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa SACCOS kwenye mikoa ya kanda ya kati ya Dodoma, Manyara na Singida.

Nyamba alisema kwa sasa tunaenda kufanya vizuri kwenye sacco zetu na viongozi wetu waende kutimiza majukumu yao kwa uhakika zaidi na kupunguza migogoro ya kifedha kwenye SACCOS zao .

Kwa upande wa washiriki wa wa mafunzo hayo wameishukuru serikali , kupitia kanuni za benki kuu tulizo jifunza zitasaidia sana katika SACCOS na kupunguza migogoro ya hapa na pale kwa viongozi wetu.

Wanachama hao wameiomba serikali kutoa leseni hizo kwa haraka ili kutatua changamoto zinazo wakabili katika SACCOS zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...