Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo la ofisi za Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma kutaokoa zaidi ya Sh Milioni 500 ambazo zilikua zikitumika kama kodi kila mwaka.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo la ghorofa mbili ambalo amesema limejengwa kwa fedha za ndani.

Amesema kukamilika huko kwa ofisi hizo tena kwa kutumia fedha za ndani kuwe ni mfano kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuiga mfano huo huku akiwaagiza pia kufuata utaratibu huo na kukamilisha kwa wakati miradi yao bila kuwa na visingizio.

Amesema wizara yake ilipatiwa ekari 11 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake ambapo wenyewe waliamua kujenga majengo mawili ya ofisi zao kwa mtindo wa ghorofa yenye ramani moja humu wakitumia mtindo huo wa 'force account' yaani fedha za ndani.

" Kwa kweli tunamshukuru sana Mhe Rais kwa kuhamishia makako Makuu Dodoma na kwa kufuata maelekezo yake tumefanikiwa kujenga majengo mawili moja likiwa la Ofisi Kuu ambalo limegharimu kiasi cha Sh Bilioni 1.6 wakati hili la TARURA mpaka likamilike litatumia takribani kiasi cha Sh Bilioni 2.7.

Nitoe maagizo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wao kuiga mfano huu wa Tamisemi na Tarura wa kutumia fedha za ndani na kukamilisha ujenzi kwa wakati kuna wengine kwenye maeneo yao wanatumia hadi Bilioni lakini jengo linatumia hadi miaka minne kukamilika," Amesema Jafo.

Kwa upande wake Meneja Matengenezo ya Barabara wa Tarura, Mhandisi Hamidu Mataka amesema wanatarajia kukabidhi jengo hilo ndani ya wiki mbili kutoka sasa kwa ajili ya matumizi.

Ameishukuru Serikali kwa kuwa nao karibu wakati wa ujenzi huo tangu walivyouanza Januari 2019 na ukiwa tayari ushakamilika kwa asilimia 98.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Tarura baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la ofisi zao linajongwa katika eneo la Tamisemi kwenye Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akikagua ujenzi wa jengo la ofisi za Tarura ambazo zimekamilika kwa asilimia 98. Jengo hilo litaanza kutumika ndani ya wiki mbili zijazo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akiwa ndani ya jengo la ofisi za Tarura lililojengwa kwenye Mji wa Kiserikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma.
 Muonekano wa Jengo la Ofisi za Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) lililofikia asilimia 98 kukamilika katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...