Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia)
akizungumza leo na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu mafanikio
yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na
umalizaji wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi
ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.
Aidha Jaji
Kiongozi aliueleza ujumbe huo kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali
yalivyowezesha usikilizaji wa mashauri ya jinai kwa haraka. Ujumbe huo
uko nchini kwa ziara ya kikazi.

Ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) na baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Jaji Kiongozi (ambaye hayupo pichani).

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia) akifafanua
jambo leo kwa ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu mafanikio
yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na
umalizaji wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi
ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.

Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bw. Waleed Malik (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.

Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bi. Debohar Isser (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo, ( wa tatu kushoto) ni Bi. Clara Maghani na (wa nne kushoto) ni Bw. Denis Biseko (wote ni wataalamu kutoka WB). (Picha na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...