WAFANYAKAZI wa Mahakama hapa Nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ikiwamo kuwashirikisha wafanyakazi na watumishi wa ngazi za chini ili kuleta tija katika kuwahudumia wananchi.

Pia wamehimizwa kujenga Utamaduni wa kutafuta maarifa na taarifa zitakazowawezesha kufanya kazi kwa ubunifu katika kuhudumia wateja wao.

Wito huo umetolewa leo, Jijini Dodoma na Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, Wakati akifungua Baraza la siku mbili la wafanyakazi wa Mahakama wanaokutana Jijini Dodoma kutathmini na kuweka malengo ya pamoja katika kuboresha ufanyaji kazi wao.

Amesema ili kufikia malengo waliojiwekea ni lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa na  kushirikiana kutoka ngazi za juu hadi ngazi za chini ili kuwa na uelewa mmoja kila linaliendelea kila mmoja awe anafahamu.

"Nilitake baraza hili kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikishana kutoka ngazi za chini mpaka ngazi za juu, muwe ni kitu kimoja kwa maendeleo na kuhakikisha jamii inapata haki zao kwa wakati" amesema Jaji Mkuu, Prof. Ibrahimi Juma.

Ameongeza kuwa "Kama watumishi wa Mahakama tuwe na utaratibu wa mara kwa mara katika kutafuta maarifa na taarifa ili kwenda na wakati kwa sababu Dunia ya sasa inabadilika kila siku hivyo lazima tujue,".

Amebainisha kuwa kwa sasa dunia imebadilika hivyo watumishi wanapaswa kusoma ili kuweza kufanya kazi kwa haki badala ya kuonea watu na kuongeza kuwa masuala ya mtandao ni muhimu kuyajua kwa sababu masuala ya tejnolojia yapo juu.

Jaji Mkuu amesema kuwa hivi sasa kuna mabadiliko makubwa katika mahakama ambapo kuna wataalam wengi jambo ambalo linaweza kurahisisha utendaji kazi kwenye muhimili huo.

Amesema katika mkutano huo wa siku mbili mada ambazo zitaongelewa zikawe chachu ya kuleta mabadiliko katika utendaji kazi katika mahakama hapa nchini.

Amesema kuna haja ya kuwashirikisha watumishi wa ngazi za chini kwa sababu Kuna wakati bajeti huwa inapanda na kushuka hivyo watumishi wanapawa kujulishwa kama bajeti inapanda na kushuka  ili wajue kama imepanda au kushuka na kuelezwa nini sababu ya kufiki hivyo.

"Hakuna sababu ya kuwaficha kuhusu mabadiliko ya bajeti na miradi inayotekelezwa, "amesema

Amebainisha kuwa majadiliano na mapendekezo ya wafanyakazi katika baraza hilo yatasaidia kuendeleza mpango mkakati wa Mahakama Katika utekelezaji wa mambo waliojipangia.

Pia amesema kuwa kwa Sasa ndani ya muhimili huo Kuna mabadiliko kwani kwa Sasa wanaowataalamu wa kada mbalimbali wa ndani Jambo ambalo Lina lahisisha utendaji kazi wa muhimili huo.

" Kwa Sasa tunawalaalamu mbalimbali wa ndani Kama Tehama,usimamizi wa maboresho, uhandisi, utunzaji wa kumbukumbu, uchumi na nyingine nyingi" amesema.

 Jaji Mkuu Nchini, Profesa Ibrahim Juma akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama katika mkutano wao wa siku mbili unaofanyika jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa Mahakama kitengo cha Masijala wakimsikiliza kwa makini Jaji Mkuu nchini, Profesa Ibrahim Juma wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi wa Mahakama linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...