Na Mwashungi  Tahir 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ameitaka jamii kutembelea vivutio vya utalii ili  kuelewa vivutio vya kitalii viliopo Zanzibar na kuachana na  dhana ya utalii kwa wageni .

Akizungumza hayo na Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baiskeli  huko Shehia ya  Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipokuwa akifunga tamasha hilo na kuitaka jamii , vijana kutembelea sehemu zenye mambo mbalimbali katika Mkoa huo.

Amesema Wazanzibar wengi wanahisi utalii uko sehemu ya Forodhani , na kuwataka waachana  na dhana hiyo, kwa kufahamu kwamba utalii uko Zanzibar nzima  na una  sehemu  nyingi za vivutio takribani vingi sana ikiwemo Mkoa wa Kusini Unguja.

“Watalii wengi wanaona utalii upo Forodhani tu, hapana, utalii uko Zanzibar Nzima na kuna vivutio vingi katika sehemu mbali mbali za Zanzibar”, Alisema Mkuu wa Mkoa huyo.

Hata hivyo amesema wazaliwa wa Nchi hii wawe wa mwanzo katika kukuza utalii wa ndani na kuutangaza Utalii kwa wote na ili uwe endelevu kwa lengo la kuuimarisha.

Aidha aliwataka Wazanzibar kuweka mashirikiano na umoja  kwa lengo la kuuweka utalii wa ndani na utalii kwa wote katika Mkoa huo.

Pia alisema katika Mkoa wa Kusini Unguja tushatekeleza kwa vitendo  dhana  hiyo ya Utalii kwa  kufanya matembezi katika maeneo mbali mbali ya kitalii yenye vivutio vyote vya Kitalii  na kuwapatia fursa vijana kuweza kujua mambo yaliyomo .

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja  Idrissa Kitwana  Mustafa amesema rasilimali zilizopo ndani ya Mkoa huo  zitawafanya vijana kuzitumia kwa kupitia ujasiriamali  na mambo mengine ya kujiendeleza kwa kupitia vivutio hivyo vya utalii.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kati  Hamida Mussa Khamis  amesema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Mapinduzi katika Sekta ya Utalii wa ndani na Utalii kwa wote kwa kufanya kwa vitendo.

Pia amesema ndani ya tamasha hilo vijana wameweza kujifunza na kuelimika kwa mambo mengi ambayo walikuwa hawayajui.

Nao washiriki wamevutika sana kwa matembezi hayo na kuahidi mwakani watajitokeza zaidi.

Zaidi ya vivutio vya utalii wa ndani na Utalii kwa wote 13 vimeweza kutembelewa na washiriki kukabidhiwa vyeti na Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tena  ifikapo Ijumaa ya mwisho January 2021 ndani ya Mkoa huo .
 Baadhi ya vitu vya asili kutoka Makunduchi,ukiwemo Msikiti Kichaka, vyakula na kupigana magomba, vilifanywa katika Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa mwakakogwa Mzee Mwita wakati wakiwa katika ziara ya Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
  Mmoja wa Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Kudrat Mussa kutoka Tanzania Bara akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
 Fundi Mkuu wa Baskeli katika msafara wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Juma Lukodwa akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli  Vuai Ali Maneno kutoka Vilabu vya Baskeli Zanzibar hafla iliyofanyika Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja .
  Sheha wa Shehia ya Cheju Bitatu akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud katika Ufungaji wa Tamasha hilo huko Kiboje Wilaya ya Kati.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Baraza la Vijana la Wilaya ya kati Baskeli na Vifaa vya kazi huko Kiboje Wilaya ya kati katika Ufungaji wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
 Baraza la Vijana kutoka Wilaya ya Kusini Unguja wakikabidhiwa Baskeli na Vifaa vya kazi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud hafla iliyofanyika Kiboje Wilaya ya kati.

                      Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...