Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MKALI wa Muziki wa hiphop kutoka kaskazini John Makini akanusha tetesi zilizozaga mitandaoni siku za nyuma kuwa alimnyima kolabo Diamond platnum.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio hapa nchini Joh Makini amesema habagui kufanya kazi na wasanii wowote na yupo tayari kufanya kazi nao na kutaka taarifa hizo zipuuzwe japo anajua kuwa nani alizisambaza mitandaoni.

"Ikitokea nimefanya kazi nae nadhani itakua nzuri kutokana na uwezo wake na ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa ndani na nje ya nchi, anatuwakilisha  vizuri,"

Pia amewapa ujumbe wasanii wachanga kuwa wafute dhana iliyojengeka kwamba msanii wakibongo ili afanye vizuri ni lazima afanye kazi na msanii mkubwa mwenye jina kutoka nje

"Tuna watu wenye vipaji ambao wanaweza kufanya chochote bila kumshirikisha mtu maarufu kutoka nje ya nchi hasa wasanii wenye majina japo sisi kama wasanii muda mwingine tunahitaji kubadilisha ladha na kuongeza mashabiki na ndio maana tunashirikisha watu hao lakini wakati mwengine sio Jambo la ulazima Sana katika kupandisha kiwango Cha msanii,"

Joh Makini ameongeza kuwa wimbo wake wa "content" ambao unafanya vizuri vituo vya redio na televisheni kwa sasa hakuutungia mistari kabla.

"Ngoma yangu mpya sikuandika mistari kabla niliingiza sauti moja kwa moja nikiwa studio na mara nyingi huwa nafanya hivyo."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...