NA ELISA SHUNDA,MONDULI.

UMOJA wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Arusha, Mwishoni Mwa Wiki, Imemkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo Taifa Ambaye Pia Ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Hicho, Dk.Edmund Mndolwa,  Shilingi Milioni Moja kwa Ajili ya Kumchukulia Fomu ya Kugombea  Nafasi ya Urais kwa Awamu ya Pili.

Akiongea wakati akimkabidhi Mwenyekiti huyo fedha hizo Katibu mwenezi wa wilaya ya Arumeru ambaye pia ni mjumbe Wa kamati ya utekelezaji wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Joshua Ongura alisema kuwa kutokana na tamko la Mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa alilolitoa December 2019 katika kongamano lililofanyika jijini Dar es salam wameona watoe fedha hizo

Alisema kuwa katika kongamano hilo jumuiya ya wazazi iliahidi kumchukulia fomu ya kugombea urais kwa awamu ya pili Mwenyekiti Wa chama hicho ambaye pia ni Rais Wa serikali ya awamu ya tano, Dk.John Pombe Joseph Magufuli.

Alisema kwa kuwa mkoa Wa Arusha unaanzia na alama A wameamua kuwa Wa kwanza kumchangia rais ,pia wameona watoe kwa kua raid ameweza kutekeleza vyema ilani ya chama ,na kutatua matatizo ya wananchi

Akiongea Mara baada ya kuipokea Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa Ambaye pia ni mjumbe Wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi  Edmund Mndolwa aliwashukuru jumuiya hiyo kwa moyo walionyesha Wa kutoa fedha kwa ajili ya kumchukulia Rais fomu ya kugombea katika kipindi kingine

Alisema  aliahidi Rais kumchukulia fomu ya kugombea katika kipindi kingine ,ambapo alisema iwapo mikoa yote itatoa fedha hizo itapatikana jumla shilingi milioni 31 ambayo katika hizo watachukuwa shilingi milioni moja ya kumchukulia fomu Rais na fedha nyingine zitaingizwa kwenye kampeni yake.

Alizitaka  mikoa mingine kuiga na kuanza kumchangia fedha ya fomu Rais kama vile mkoa Wa Arusha ulivyofanya na ulivyoanza kutoa fedha hizo mapema.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Ambaye Ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Hicho, Dk.Edmund Mndolwa, Akipokea Fedha Tsh.Milioni Moja Kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo Mkoa wa Arusha, Hezron Mbise (Kulia) kwa Ajili ya Kumchukulia Fomu ya Urais kwa Awamu ya Pili, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais, Dk.John Pombe Joseph Magufuli, Baada ya Kumaliza Kufungua Baraza la Mkoa Huo Lililofanyika Wilayani Monduli, Mwishoni Mwa Wiki. Katikati Ni Katibu Mkuu wa Jumuiya Hiyo, Mwalimu, Erasto Sima. Picha na Elisa Shunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...