Jumuiya
ya Afrika mashariki imeshauriwa kubuni vyanzo vya mapato
vitakavyoiwezesha kujiendesha bila kutegemea Michango inayotolewa
na nchi wanachama na pia wafadhili
Mjadala
huo uliibuka wakati wabunge wakichanganua ripoti ya ukaguzi wa
mahesabu za jumuiya a hiyo baada ya mbunge kutoka Uganda suzan
Nakawuki kulieleza Bunge kuwa kuna haja ya hatua za kisheria kuanza
kuchukuliwa kwa idara ama watendaji wasiotimiza wajibu wao na
kusababisha baadhi ya matatizo kujirudia
Hata
hivyo hoja hiyo pamoja na hoja hiyo kuwa na lengo ka
kufanikisha mipango na kufikia malengo , baadhi ya wabunge akiwemo
pamela maasai kutoka Tanzania wamesema kutumia sheria ama katika
suala hilo hakutakuwa na tija kwani kimsingi masuala mengi ya
jumuiya yanaendeshwa kwa mfumo wa majadiliano ,kushauriana na
kuvumiliana
Aidha
pia mbunge huyo akatoa mapendekezo kwa jumuiya kuangalia upya
namna ya kupata fedha za kujiendesha bila kutegemea michango ya
nchi wanachama kwa asilimia kubwa na pia ile inayotolewa na
wafadhili .
Mariamu
Ussi ni Mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania anabainisha baadhi
ya athari zinazojitokeza kutokana na ukosefu wa fedha za
kutosha ikiwemo ya jumuiya kushindwa kukidhi mahitaji muhimu
yakiwemo ya wafanyakazi.
Tatizo
la ukosefu wa fedha katika Jumiya ya Afrika mashariki limekuwa
likijitokeza mara kwa mara na kulalamikiwa na wabunge wa bunge hilo
na pia licha ya kuwa limekuwa likishughulikiwa baadhi ya wabunge
wanasema kasi yake ni ndogo .
Jumuiya
hiyo ya afrika amashariki inayoundwa na nchi sita za Tanania Kenya
,Uganda , Rwanda ,Burundi na sudani kusini ikikadiriwa kuwa na watu
wapatao milioni 173 kwa asilimia kubwa inaendeshwa kwa michango
inayotolewa na nchi wanachama na pia inayotolewa na wafadhili .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...