Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmond Mndolwa akikata utepe wakati wa kukabidhi mashine ya kufyatua matofali wakati alipotembelea halmashauri ya wilaya ya Longido.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Edmond Mndolwa akikabidhi viti wakati alipotembelea halmashauri ya wilaya ya Longido.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmond Mndolwa akizungumza wakati akikabidhi mashine ya kufya tua matofali wakati alipotembelea halmashauri ya wilaya ya Longido.

Na Woinde Shizza, Arusha 
MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk Edmond Mndolwa amesema mradi wa nyuki ulioanzishwa na jumuiya hiyo unatakiwa kuanzishwa pia na jumuiya nyingine za chama hicho.

Akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya Longido jana  Dkt Mndolwa amesema mradi wa nyuki ni kitega uchumi ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa muda mfupi hivyo ni vyema jumuiya nyingine zikaanzisha mradi huo ikiwemo UVCCM na UWT.

Amesema mradi huu wa Nyuki utasaidia kuongeza ajira katika nchi yetu na utasaidia kuwaondoa vijana wengi vijiweni kwani wataweza kujiajiri wenyewe ,aidha alibainisha kutoka na hilo ataenda kuishauri kamati ya chama chake kuingiza mradi huu Wa Nyuki katika ilani ya uchaguzi ili uwe mradi Wa Taifa.

"Mradi wa nyuki ni mradi wenye tija na nitahakikisha unaongia kwenye rasimu yetu ya ilani ili uwe sehemu ya miradi itakayotekelezwa na Serikali mahususi kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana hawana ajira ili waweze kujiajiri kupitia mradi huo".

Amesema  kwa sasa soko la asali ni kubwa sana duniani na pia bei ni kubwa tofauti na zao lingine  lolote lile  kwani  kwa sasa lita moja ya asali inafika shilingi elfu 12 wakati bidhaa zingine kama mchele ni shilingi 2500, sukari ni shilingi 2600 na hiyo inaonyesha tu kuwa asali ni zao ambalo linaela kuliko mazao mengine yoyote Yale.

Aidha katika ziara hiyo ya utekelezaji wa wa ilani , ameweza kukabidhi
Mashine ya kufyatulia matofali yenye thamani ya shilingi milioni sita na lakimoja ,viti vya plastiki 100 vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu  pamoja na mizinga ya Nyuki 100 yenye thamani ya shilingi milioni 20 vitu vyote hivi vikiwa vimetolewa na Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha Hezron mbise.

Amempongeza Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha kwa kutoa bidhaa hizo ambapo aliwataka viongozi wengine waige mfano wake huku akiwaonya wagombea ambao ni wanachama wa chama cha mapinduzi wanaoenda kugombea nafasi mbalimbali wasithubutu kuhonga ilo wapate nafasi.

"Napenda kuwaomba wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani ,kutohonga wananchi fedha badala yake wahonge chama cha mapinduzi  kwa kuwaletea maendeleo, huku akibainisha iwapo atabainika mtu alieonga binadamu  hatachukuliwa hatua ikiwemo kukatwa jina lake" amesema Mndolwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Longido, Josefu Sadala ameshukuru jumuiya hiyo kwa kuwapa miradi hiyo nakuhaidi kuwa wataitunza na kuisimamia vyema ,uku akibainisha  kuwa vitu hivi vitasaidia kuwapa ajira vijana Wa wilaya  hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...